Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-: Picha muongo ya nyumba inayodaiwa kuwa ndiyo aliyokuwa akiishi Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, imeenea katika mitandao ya kijamii na kuzua maoni mbalimbali kuhusu maisha yake ya unyenyekevu.
Maelezo yanayoambatana na picha hiyo yanasema: "Katika nyumba hii aliishi mtu aliyetoa maisha yake katika nyanja zote za jihadi; Kiongozi Mkuu, Sayyid Ali Khamenei."
Wachambuzi na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wameeleza kuwa unyenyekevu wa makazi hayo unaakisi mtindo wa maisha wa viongozi wanaoweka mbele huduma kwa dini na jamii badala ya anasa za dunia.
Aidha, maelezo hayo yanasisitiza kuwa watu wanaojitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu huamini kwamba maisha ya dunia ni ya muda mfupi, huku thawabu na hadhi ya Akhera ndiyo yenye kudumu milele.
Your Comment