Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Vyombo vya habari vya Uturuki vimeripoti kuwa ibada ya kusalia mwili wa Kiongozi Shahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ali Khamenei, imefanyika katika Msikiti wa Imam Khomeini mjini Tehran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Anadolu, hafla hiyo iliongozwa na Ja'far Sobhani na kuhudhuriwa na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, pamoja na viongozi mbalimbali wa kisiasa, kijeshi na kidini wa nchi hiyo, huku maelfu ya wananchi wakishiriki katika ibada hiyo ya maombolezo.

Sherehe hiyo ya sala ya maiti ilifanyika katika mazingira ya maombolezo makubwa, ambapo wananchi walikusanyika kwa wingi kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo shahidi.

Your Comment