5 Julai 2026 - 20:47
kamanda wa jeshi la majini la Iran: muqawama haujafungwa tena na mipaka ya kijiografia

Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran, Admiral Shahram Irani, amesema kuwa Muqawama sasa umevuka mipaka ya kijiografia, akisisitiza kuwa mataifa na vikosi vya Muqawama vinaendelea kuimarisha umoja na mshikamano katika kukabiliana na changamoto.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Admiral Shahram Irani, amesema kuwa Muqawama haujafungwa tena ndani ya eneo maalumu la kijiografia, bali umekuwa harakati pana inayowaunganisha watu huru katika mataifa mbalimbali.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Masirah cha Yemen, Admiral Irani alisema kuwa adui kwa sasa anakabiliana na Uislamu wenye nguvu pamoja na Muqawama wa Kiislamu, akieleza kuwa mataifa na vikosi vya Muqawama vimeongeza mshikamano na umoja wao katika kukabiliana na changamoto zilizopo.

Aidha, alisema kuwa mamilioni ya washiriki katika shughuli za mazishi walifanya upya ahadi yao ya kuendelea kushikamana na njia ya viongozi wao, wakisisitiza maadili ya udugu, umoja na kujitolea.

Kamanda huyo aliongeza kuwa watoto na wafuasi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyefariki kishahidi walikusanyika ili kuthibitisha uaminifu wao kwa misingi na mafundisho waliyojifunza kutoka katika shule yake ya fikra na uongozi, wakiahidi kuendeleza njia hiyo kwa uthabiti.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha