11 Julai 2026 - 09:54
Shule ya Wasichana Yaadhimisha Shahada ya Imam Sajjad (a.s.) kwa Majlisi ya Maombolezo +Picha

Majlisi ya maombolezo ya kumbukumbu ya shahada ya Imam Ali ibn al-Husayn As-Sajjad (a.s.) imefanyika katika Shule ya Wasichana, ambapo washiriki 144 walihudhuria na kupata mawaidha kuhusu maisha, subira na urithi wa Imam wa Nne wa Ahlul-Bayt (a.s.).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) – ABNA – Hawzah ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa), iliyopo Kigamboni - Dar-es-salaam imeandaa Majlisi ya Maombolezo kwa mnasaba wa kumbukumbu ya Shahada ya Imam wa Nne wa Ahlul-Bayt (a.s.), Imam Ali ibn al-Hussein As-Sajjad (a.s.), siku ya Ijumaa, tarehe 10 Julai 2026.

Shule ya Wasichana Yaadhimisha Shahada ya Imam Sajjad (a.s.) kwa Majlisi ya Maombolezo +Picha

Majlisi hiyo ilifanyika katika mazingira ya ibada na maombolezo, ambapo Bi. Rizq Yahya alitoa muhadhara ulioangazia maisha ya Imam Sajjad (a.s.), nafasi yake katika kuhuisha mafundisho ya Uislamu baada ya tukio la Karbala, pamoja na mafunzo ya subira, ibada na maadili yanayopatikana katika historia yake.

Jumla ya washiriki 144 walihudhuria majlisi hiyo, wakiwemo wanafunzi wa kike pamoja na wasimamizi wao. Washiriki walipata fursa ya kukumbushwa umuhimu wa kushikamana na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s.) na kuiga mwenendo wa Imam Sajjad (a.s) katika ibada, uchamungu na uvumilivu.

Majlisi hiyo iliandaliwa na Hawzah ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa), ikiwa ni sehemu ya kuendeleza utamaduni wa kuwakumbuka Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.) na kuimarisha malezi ya kiroho kwa wanafunzi.

Shule ya Wasichana Yaadhimisha Shahada ya Imam Sajjad (a.s.) kwa Majlisi ya Maombolezo +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha