Rais wa Syria ameyasema hayo katika mahojiano aliyofanywa na gazeti la Uingereza la Suday Telegraph al na kuongeza kwamba kamwe Syria haiwezi kufanywa Afghanistan nyingine na kuongeza kuwa tatizo lolote litakaloikabili Syria litazusha matatizo katika eneo lote la Mashariki ya Kati.Rais wa Syria amesisitiza kwamba serikali yake imejitahidi kufanya mabadiliko nchini humo na kuzionya nchi za Magharibi kuwa zisiingilie masuala ya ndani ya nchi hiyo.Wakati hayo yakiripotiwa askari 20 wameripotiwa kuuawa katika mji wa Homs nchini Syria na wengine 53 kujeruhiwa katika mapigano yaliyotokea kati yao na wanamgambo wenye silaha.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 275504
Rais Bashar al Assad wa Syria amezionya nchi za Magharibi kutothubutu kuishambulia nchi yake na kusema kuwa zikifanya hivyo zitakabiliwa na zilzala.