19 Machi 2011 - 20:30

Shekh wa Azhar atenga mfuko wa fidha kwa lengo la kuipatia uhuru Miri kutoka kwa wamarekani, nakusema kuwa misaada ya marekani kwa Miri, ni njia ya kuibana Misri ambapo haikubaliki kwa wamisri.

Shekh Ahmad Atwibu amesema: mfuko huo ni malumu kwaajili ya kuuhami uchumi wa taifa la Misri, na kwaajili ya uhuru na kujitegemea kutokana na misaada ya kiamerika, misaada ambayo inasababisha kubanwa nchi hiyo kutoka kwa wamarekani. Nae amewataka wamisri wote walio ndani na nje ya nchi kusaidia mfuko huo. Hatua hii ya Shekh wa Azhar imepokelewa vyema na makundi yote ya kiislamu kamavile masalafia na masufia na wengineo, na yaasemekana kuwa mfuko huo utaitwa umfuko wa ukarimu na utukufu. Na msimamizi wa mfuko huo atakuwa ni Shekh wa Azhar, wakuu wa kisiasa, viongozi wa Dini ya kiislamu na kikiristo, shahsia za heshima na wataalamu wa uchumi wa nchi hiyo.