Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Geoget Lopal ajuza mwenye umri wa miaka 90 alisilimu na kubadili jina kuitwa Nuur, Mama huyo ni mkazi wa Flander Belgium, kwa ripoti hii Mama huyu ni wa kwanza kusilimu kuwa na miaka mingi na kuvunja rekodi ya dunia.
Sababu ya kusilimu Mama huyu ni kuvutiwa na tabia nzuri ya Waislamu duniani hasa majirani zake, akisema: Mara nyingi nashuhudia majirani zangu kuwa pamoja na muamala baina yao hauna kifani, na kila siku humuabudu Mwenyezi Mungu na kuomba Dua kwa pamoja, na wameshikamana na itikadi yao, kwa itikadi yao hiyo huasababisha kuwa madhubuti na kuwa na uhusiano mzuri wa kifamilia, tofauti na sisi, familia yangu hasa Mtoto wangu wa kike yapita siku na miezi bila kunijulia hali yangu ila majirani zangu kila siku wanijulia hali.
Akiendelea kusema: Mimi kila siku nilikuwa nataraji kujua itikadi ya majirani zangu na Dini yao na hii ilikuwa sababu ya kuvutiwa nao.
Nuur alikiishi na Waislamu katika nchi ya Moroco mwezi wa Ramadhani na baada ya kushuhudia tabia ya Waislamu alichagua Uislamu kuwa Dini yake, na kwa sasa ashiriki katika masomo tofauti ili kuujua Uislamu zaidi, na haki za Wanawake katika Uislamu.