ndege hiyo ambayo ni ndege ya kizazi cha pili iliyotengenezwa na jeshi la Iran itazinduliwa na rais wa Iran Dakta Ahmad Nejad.
ni muhimu kuashiria kuwandege hiyo ya jet ni ndege iliyotengenezwa na jeshi la Iran kwa teknolojia ya wairan, jeshi la Iran lilianza shughuli za kutengeneza silaha binafsi, katika kipindi cha vita na Iraq mwaka 1980 mpaka 1988 ambapo Iraq ikishirikiana na Marekani waliivamia Iran.
kufika mwaka 1992 Iran ilitengeneza kifaru chake cha kwanza na mpaka leo hii Iran inajitegemea katika nyanja zote za kijeshi.