Rais Bahsar al-Assad wa Syria jana amesema, ingawa Syria inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya kigaidi lakini kutokana na uungaji mkono wa wananchi wa Syria kwa jeshi la Syria, sasa hali ya mapambano dhidi ya kundi la wapinzani imekuwa nzuri siku hadi siku. Wakati Syira inaposukuma mbele mageuzi ya kisiasa, itapambana vikali zaidi na ugaidi wa aina mbalimbali.
Gazeti la Vatan gazetesi la serikali ya Syria siku hiyo limesema kuwa, jeshi la serikali la Syria limepambana vikali na wapiganaji waasi na kufanikiwa kudhibiti vijiji vitano muhimu katika eneo la mpaka wa Syria na Lebanon, na mamia ya wapiganaji wameuawa.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid Al-Moualem jana amekutana na mwenyekiti wa kamati ya usalama wa taifa na sera za kidiplomasia ya bunge la kiislam la Iran Alaeddin Boroujerdi. Katika mkutano huo, Al-Moualem amesema, mkutano wa Marafiki wa Syria uliofanyikia tarehe 20 ulilenga kupunguza ushawishi wa Syria katika eneo la Mashariki ya Kati. Ameongeza kuwa Syria inapinga nguvu zote za nje kuingilia mambo ya ndani ya nchi hiyo.