Ripoti ya shirika la habari Ahlul Bayt(as)-ABNA- Baada ya kutendewa vitendo vibaya Wanawake wa Saudia kuamua kuandaa tangazo la kuonyesha nini yanayojiri dhidi ya Wanawake hao.
CNN imeripoti na kusambaza picha ya Mwanamke alovaa vazi la Kisaudia huku jicho lake moja likiwa limebadilika rangi baada tu ya kupigwa kipigo kikali.
Katika picha ya tangazo hilo kumeandikwa; baadhi ya mambo hayawezekani kuyaficha, shuhudieni nini wafanyiwa Wanawake nchini Saudia sasa twahitaji mapinduzi.
Picha ya tangazo hili imeandaliwa na Taasisi ya Malik Khalid ili kupambana na vitendo vibaya dhidi ya Wanawake. Taasisi hii iliasisiwa mwaka 2001 na watoto wa mfalme Malik Khalid alokuwa mfalme wa Saudi Arabia mwaka 1975 – 1982.
Hii ni kwa mara ya kwanza Taasisi za familia za kifalme kufanya kitendo kama hicho kuonyesha dhuluma inayofanywa nchini humo dhidi ya Wanawake.
Jumuiya na Taasisi tofauti za Kimataifa za pinga vikali matendo mabaya yanayofanywa Saudi Arabia dhidi ya Wanawake wa nchi hiyo, Wanawake Saudi Arabia hawana haki ya kuendesha gari au kutoka nje bila kuwa na watu wa baribu yao.
