12 Oktoba 2013 - 20:30
Kamwe uranium haitasafirishwa nje

Mwakilishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia Abbas Araqchi amesema Iran kamwe haitasafirisha nje uranium nzito wala kusimamisha shughuli ya kusafisha uranium nzito.

 Ripoti ya ABNA- Akizungumza leo, Bw Araqchi amesema usafishaji wa uranium nzito ni "mstari wa mwisho" kwa Iran kwenye mazungumzo, na kusisitiza kuwa Iran haitalegeza msimamo hata kidogo kuhusu haki yake ya matumizi salama ya nyuklia kwa mujibu wa kanuni za kimataifa.  

Mazungumzo kati ya Iran na nchi tano zenye uwezo mkubwa zaidi duniani ambazo ni Uingereza, China, Ufaransa, Russia, Marekani na Ujerumani yalifanyika mara mbili huko Almaty, Kazakhstan mwezi Februari, na kushindwa kufikia maendeleo yoyote halisi.

Hivi sasa mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika tena mjini Geneva Uswizi kati ya tarehe 15 na 16 mwezi huu.  

Araqchi, ambaye pia ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran, amesema Iran itahudhuria mazungumzo hayo kwa makini na itajitahidi kutimiza lengo dhahiri litakalokubaliwa na pande zote.