Mwenyekiti wa Hizbullah amesema kuwa Jeshi lake litapambana na magaidi kwa nguvu zote.
Sayyid Hasan Nasrullah ameyasema hayo alipotembelea maeneo ya mashariki mwa Lebanon sehemu ambayo makundi ya kigaidi yanafanya mashambulizi.
Aliendelea kusema kuwa Hizbollah ina nia ya kupambana na magaidi na Inshallah tutafikia lengo letu.
Pia aliashiria kwamba Jeshi la Hizbollah huwa halina desturi ya kusalimu amri.
Alimalizia kwa kusema, Stahamala,kujidhatiti na uvumilivu ndio siri ya mafanikio, somo hili tumelipata kupitia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ilistahamili na kujidhatiti katika vita vya miaka minane na hatimaye kushinda vita hivyo.
Wachambuzi wanasema kuwa safari hii ya Sayyid Hassan Nasrullah ya kutembelea maeneo ya mapambano, itawapa moyo wapambanaji wa Hizbollah katika kupambana na magaidi huko Syria na Lebanon.
14 Oktoba 2014 - 10:40
News ID: 644250

Mwenyekiti wa Hizbullah amesema kuwa Jeshi lake litapambana na magaidi kwa nguvu zote.