12 Novemba 2014 - 16:48
Ajali a basi yaua watu wanne

Watu WANNE wamefarikini dunia, na wengine AROBAINI kujeruhiwa katika ajli ya Basi la WIBONELA

Watu WANNE wamefarikini dunia, na wengine AROBAINI kujeruhiwa katika ajli ya Basi la WIBONELA, lililokuwa likitokea mjini KAHAMA, mkoani SHINYANGA kuelekea jijini DAR ES SALAAM.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema basi hilo lilishindwa kukata kona ya kuingia barabara kuu na kupinduka zaidi ya mara moja kutokana na kuwa katika mwendo kas.i
Kamanda wa POLISI wa mkoa wa SHINYANGA, JUSTUS KAMUGISA amethinitisha kutokea kwa ajali hiyo na kukiri kuwa chanzo kikuu cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
Mganga mfawidhi wa Hospitali ya mji wa KAHAMA Dokta JOSEPH NGOWI amesema majeruhi wanaendelea vizuri na matibabu huku miili ya marehemu imehifadhiwa katika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali hiyo.
Tanzania imekuwa ikikabiliwa na ajali za mara kwa mara, kutokana na ubovu wa barabara na uzembe, na kutozingatiwa kanuni za barabarani.