20 Novemba 2014 - 17:43
Putin aapa kutoruhusu nguvu za nje kuiharibu Taifa lake

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi yake itafanya kila iwezalo kujilinda dhidi ya siasa kali na kuzuia kile alichokiita "mapinduzi ya rangi".

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi yake itafanya kila iwezalo kujilinda dhidi ya siasa kali na kuzuia kile alichokiita "mapinduzi ya rangi".
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Usalama la nchi yake hivi leo, ameonya dhidi ya kutumia ajenda ya siasa kali kama nyenzo ya mataifa mengine kujitanua na kwamba nchi yake haitaruhusu wimbi la mageuzi linalochochewa na mataifa ya nje kuathiri utangamano uliopo. Wakati huo huo, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, ameikosoa vikali siasa ya Urusi kuelekea Ukraine, akiita ni "kanuni ya mwenye nguvu mpishe." Akizungumza mjini Swidnica, kusini magharibi mwa Poland, hivi leo, Merkel amesema hata hivyo Ujerumani itaendelea kujadiliana na Urusi. Kansela huyo alikuwa akishiriki kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya ushirikiano wa Poland na Ujerumani akiwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ewa Kapozc.

Tags