Polisi nchini Niger imefyatua gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa chama cha upinzani waliokuwa wamekusanyika kuandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Niamey hii leo licha ya onyo kutoka kwa serikali dhidi ya kuandamana kupinga utawala mbovu.Gavana wa Niamey alikuwa amepiga marufuku maandamano hayo siku ya Ijumaa kabla ya maandamano ya ghasia kuzuka nchini humo kutoka kwa waumini wa kiislamu walioghadhabishwa na kuchapishwa kwa kikaragosi cha mtume Muhammad katika jarida maalum la gazeti la Ufaransa Charlie Hebdo ambayo yamesababisha makanisa kadhaa na vilabu vya burudani kuchomwa huku kiasi ya watu kumi wakiuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ghasia hizo. Mbali na hali ya taharuki kuibuka kutokana na machafuko hayo ya kidini, kumekuwa na hali tete kisiasa nchini Niger tangu mwaka 2013 baada ya mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa Hama Amadou kujiondoa kutoka chama tawala baada ya kutofautiana na Rais Mahamadou Issoufou.
Kitendo cha serikali ya Ufaransa kuunga mkono kudhalilishwa mtume Muhammad s.a.w kumewaudhi waumini wa dini ya kiislamu na kusababisha kuwa na mtazamo mbaya kwa serikali hiyo.