Shirikala la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: ndege za kijeshi za Saudi Arabia zikishirikia na nchi kume ikiwemo nchi tano za Baraza la ushirikiano la Ghuba ya Uajemi (ispokuwa nchi ya Oman) yameanza mashambuli ya anga nchini Yemen, katika mashambulio hayo mpaka sasa watu zaidi ya 18 wamepoteza maisha na wengi kujeruhiwa.
Katika uvamizi huo ulioanza usiku wa jumatano zimeshiriki ndege 30 kutoka umoja wa falme za kiarabu, 15 kutoka kuwait, 6 kutoka Morocco zikiwemu meli zakivita za Misri na Pakistani.
Mashambulizi hayo zaidi yamelenga maeneo ya makazi ya watu yaliopo karibu na uwanja wa ndege wa Sana`a pia majengo na ofisi za serikali na kambi ya jeshi la anga la Daylamiy nchini humo.
Pia ripoti zinaeleza kuwa ndege za Saudi Arabia zimearibu ofisi moja ya Mahuthi mjini Sana`a kitu ambacho kimepealea maafa makubwa ya vifo vya watu katika mashambulio hayo, hivyo kwamujibu wa ripoti ya vikundi vya uokoaji mpaka sasa juhudi za kuokoa miili ya walifunikiwa na kifusi katika jengo bado zinaendelea.
Saudi Arabia yaeleza sababu kuu iliopelea kuchukua maamuzi hayo nikile walichokisema kuwa ni amani ya sehemu hiyo (kwamaana kama mahuthiy watashika mamlaka ya uongozi wa taifa la Yemen) wao hawatakuwa na amani.
Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani alipokuwa akifanya maojiano na vyombo vya habari nchini humo alisema: vita nihatua ya mwesho yakufikia malengo nasi bila yakupenda tumeamua kuchukua hatua hiyo.
Aidha aliongeza kusema: tutakachotumia kuwazuia mahuthiy wa Yemen wasiitawale Yemen ni makubaliano hayo ya nchi hizo kumi.
Nchi zilioshiriki katika makubaliano hayo ni Umoja wa Falme za kiarabu, Kuwait, Morocco, Qatar, Bahrain, Misri, Pakistani na...
Marekani imeunga mkono uvamizi huo lakini imesema jeshi lake halitashiriki katika mashambulio hayo, habari zisio thibitishwa zaeleza kuwa kikundi cha Ansarullah nchini humo kimetangaza kuwa: kamwe hakitakaa kimya kuhusu uvamizi huo bali kitajibu mashambulio hayo katika mipaka ya Yemen na Saudi Arabia.
Kamati ya mapinduzi ya Yemen imewataka wananchi kuandamana kupinga uvamizi wa umoja huo nchini Yemen katika mkoa yote, vilevile mkuu wa kikundi cha Ansarullah amesema: watalipiza mauaji wanayoyafanya dhidi ya taifa hilo.
Televishen ya Almasirat ya Yemen emetangaza kuwa baada ya masaa kadhaa yajayo utatolewa wito wakuwataka wananchi kushiriki katika vita dhidi ya Saudi Arabia, nahapo ndipo patafahamika ushindi utakuwa kwanani?.
26 Machi 2015 - 22:25
Msimbo wa Habari: 679239
Wizra ya afya na ulinzi nchini Yemen vyaeleza kuuwawa watu 18 na wengine 24 kujeruhiwa kutokana na mashambulio ya ndege za makubaliano ya nchi kumi yakuvamia Yemen yakiongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Mahuthi nchini humo