2 Aprili 2015 - 08:55
 Israel yafanyia majaribio makombora mapya

Serikali ya Marekani yaipatia Israel makombora mapya ya ulizi wa anga.

Serikali ya Marekani yaipatia Israel makombora mapya  ya ulizi wa anga.

Wizara ya ulinzi ya Israel imesema kwamba mfumo mpya wa ulinzi wa anga ambao umeundwa kwa ushirikiano na Marekani unaweza kuanza kutumiwa mwaka ujao.

Mfumo huo ujulikanao kama David's sling, au 'Manati ya Daudi' ulifanyiwa majaribio jana na uliweza kudungua makombora ya masafa marefu ya kuigiza ambayo yanaweza kufyatuliwa kutoka Syria au Lebanon. Tangazo la majaribio ya mfumo huo lilitolewa wakati makubaliano ya msingi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yakijadiliwa katika mji wa Lausanne nchini Uswisi.

Israel inaogopa uwezo wa kijeshi wa Iran, kwani Iran inaweza kuishambulia Israel bila ya kupeleka jeshi lake mipakani wa Israel, kwani inamakombora ya kuvuka hata mabara, jambo linaloikosesha usingizi serikali ya Israel na Marekani.