Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA; mmoja kati ya wanajeshi wa Iraq ametoa habari ya kuingia kwa majeshi ya Iraq ndani ya mji wa Musol.
Aidha ameashiria kusonga mbele kwa majeshi ya Iraq katika mji wa Musol na kusisitiza kuwa: majeshi ya Iraq baada ya mapambano makali ya wiki mbili mfululizo pembezoni mwa mji huo, wamefanikiwa kuingia katika mji huo, ambapo sasa wamefanikiwa kuingia katika mji huo ambao ni makao makuu ya kikundi cha kigaidi cha Daesh, huku akisisitiza kuwa mpaka sasa mapambano hayo bado yanaendelea baina ya majeshi ya Iraq na magaidi wa Daesh katika sehemu ya Alkaramah mjini Musol.
Maelfu ya majeshi ya Iraq yalishiriki mashambulizi makubwa ya wiki mbili kwaajili ya kuikomboa wilaya ya Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh, ambapo kufuatia mashambulizi hayo makali majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuvikomboa vijiji vingi viliopo nje ya Musol na kuangamiza mamia ya magaidi wa kikundi cha kigaidi Daesh katika wilaya hiyo.
mwisho wa Habari/290
1 Novemba 2016 - 20:09
Msimbo wa Habari: 789251
Majeshi ya Iraq yamefanikiwa kuwasili sehemu ya Alkaramah katika wilaya ya Musol