31 Desemba 2016 - 17:45
Bomu laripuka mjini Istambul Uturuki

Bomu hilo limeripuka sehemu ya “Maltepe” katika mji wa Istambul nchini Uturuki

Shirika la habari AhlulByat (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Uturuki vimetangaza kuwa bomu hilo limeripuka katika sehemu ya “Mltepe” katika jiji la Istambul.
Tuvuti ya gazeti la (Yenisafak) imetoa taarifa kuwa mripuko huo umetokea mjini Istabul karibu na mgahawa mmoja sehemu hiyo.
Mpaka sasa idadi ya waliofariki kufuatia tukio hilo bado haijatangazwa.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Uturuki vimetangaza kuwa katika mripuko huo mtu yeyote hajapatwa na maafa.
Picha zilio sambazwa zinaonyesha kuwa jeshi la Polisi la Uturuki limeizingira sehemu ya tukio hilo.  
mwisho/290