Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump ambaye anasadikiwa akuwa chanzo cha kuchochea chuki za mataifa ya kiarabu dhidi ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran amesema kwamba viongozi wa Mashariki ya kati walilalamika kuhusu Qatar wakati rais huyo alipotoa mwito kwa mataifa ya kiarabu kuendelea kuitenga Iran ambayo inazisaidia serikali za Iraq na Syria kupambana na magaidi wanaoungwa mkono na Marekaini na Umoja huo wa kiarabu. Kupitia ujumbe wa Twitta leo hii Trump hakuonesha anasimama upande gani kuhusiana na uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia na nchi nyingine tatu za kiarabu wa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Qatar lakini ameonekana kuonesha kwamba hatua hiyo ya mshirika wake Saudi Arabia inaeleweka.Jana Jumatatu Saudi Arabia pamoja na Bahrain,Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu zilivunja uhusiano wake na Qatar kuhusiana na madai kwamba nchi hiyo inaunga mkono magaidi .Nchi zote hizo ni marafiki wa Marekani hali ambayo imeonekana kumuweka katika nafasi ngumu rais Trump.
Mwisho wa habari / 291