9 Juni 2019 - 07:47
Ushindi wa mtawalia wa Answarullah na Jeshi la Yemen; mwanzo wa mabadiliko ya mlingano katika vita vya Yemen

Katika wiki za hivi karibuni, vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen na jeshi la nchi hiyo vimepata ushindi mbalimbali muhimu katika medani ya vita dhidi ya muungano vamizi wa Saudi Arabia.

(ABNA24.com) Katika wiki za hivi karibuni, vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen na jeshi la nchi hiyo vimepata ushindi mbalimbali muhimu katika medani ya vita dhidi ya muungano vamizi wa Saudi Arabia.

Mwanzoni mwa mwaka wa tano wa vita vya Saudi Arabia iliyokusanya kundi la baadhi ya nchi za Kiarabu na kuivamia kijeshi Yemen, wananchi wa Yemen wamezidi kuonesha kuwa wako imara tofauti na dhana zisizo na mahesabu mazuri za wavamizi wa nchi hiyo. Katika kipindi cha kuanza mwaka huo wa tano wa vita vya Yemen, jeshi la nchi hiyo kwa kushirikiana na kamati za kujitolea za wananchi limechukua hatua mbili muhimu zenye mafanikio makubwa. Ya kwanza ni kushambulia kwa makombora ya belestiki shirika kuu la mafuta la Saudi Arabia yaani Aramco. Shambulizi hilo limetia hofu kubwa katika nyoyo za Aal Saud kiasi kwamba moja ya sababu za Saudia kuitisha vikao vitatu huko Makkah ni shambulizi hilo. Hata katika hotuba zake kwenye vikao hivyo, mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia aligusia shambulizi hilo.

Hatua ya pili ni ile iliyofanywa wiki moja iliyopita na jeshi la Yemen pamoja na kamati za kujitolea za wananchi wa nchi hiyo. Yahya Sarii, msemaji wa Jeshi la Yemen na Answarullah alisema siku ya Jumatano kwamba vikosi vya Yemen katika kipindi cha masaa 72 yaliyopita vimefanikiwa kudhibiti zaidi ya kambi 20 za kijeshi za Saudi Arabia katika eneo la Najran la kusini mwa Saudia. Pigo kubwa zaidi la kijeshi kwa ukoo wa Aal Saud ni kwamba hayo yamefanyika kwa kushtukiza na bila ya kugunduliwa na majasusi wote wa kieneo na kimataifa wanaoisaidia Saudi Arabia. Ni kutokana na kushtukizwa hivyo ndio maana Saudi Arabia imepoteza pia wanajeshi wake wengi kwenye operesheni hizo. Yahya Sarii amesema, askari wengi wa Saudia wamekumbwa na hofu kubwa kutokana na operesheni hizo za kushtukia kiasi kwamba zaidi ya askari 200 wameuawa na kujeruhiwa na wengine kufanywa mateka.

Operesheni mpya zilizofanywa na jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Yemen zina sifa zake nyingine za kipekee. Operesheni hizo zimefanywa katika maeneo ya Najran na Jizan, ndani ya ardhi Saudi Arabia, katika mpaka wa nchi hiyo na Yemen. Kwa maneno mengine ni kwamba vikosi vya Yemen vimeweka kambi katika maeneo ya mpakani mwa Saudi Arabia lakimni Riyadh na kundi lake wanashindwa kukabiliana navyo.

Suala jingine ni kwamba, operesheni hizo zilizojumuisha pia mashambulizi ya kushtukiza ya makombora zimefanyika kutimiza ahadi zilizotolewa na kiongozi wa Answarullah, Abdul Malik al Houthi aliyesema mwanzoni mwa mwaka wa tano wa vita vya Yemen kwamba mwaka huu ni wa ushindi kwa wananchi wa nchi hiyo. Msemaji wa Jeshi la Yemen na Answarullah amesema: Operesheni hizo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na kiongozi wa Answarullah ambaye aliahidi kuwa mwaka wa tano wa vita vya Yemen utakuwa mwaka wa ushindi wa wananchi wa nchi hii.

Ukweli ni kwamba katika siasa zao mpya, jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa Yemen zimetoka katika sura ya kujihami tu, na sasa zimeingia katika hatua mpya ya kuanzisha mashambulizi na kutosubiri kushambuliwa ndipo wajibu. Jambo hilo linaonesha kuanza mabadiliko mapya katika mlingano wa vita vya Yemen.

Amma nukta nyingine muhimu ni kwamba, ushindi huo wa jeshi na Answarullah ya Yemen umepatikana katika hali ambayo uungaji mkono wa madola ya kibeberu kwa muungano vamizi unaoongozwa na Saudia si tu haujapungua, lakini hata umeongezeka licha ya upinzani mkubwa wa walimwengu. Ni hivi karibuni tu ambapo dola la kikoloni la Ufaransa lilitangaza kuongeza kwa asilimia 50 kiwango cha silaha ambazo Paris iliiuzia Saudia mwaka 2018 licha ya jambo hilo kukanyaga sheria zote za kimataifa.

/129