19 Juni 2019 - 09:39
Muqawama mbele ya Marekani; taifa la Iran litapata ushindi katika vita vya irada

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mapambano au muqawama ndio njia pekee ya kukabiliana na adui na kuongeza kuwa: "Mapambano ni njia pekee ya kupata ushindi mbele ya sera za Marekani, na ushindi wa taifa la Iran uko karibu."

(ABNA24.com) Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema mapambano au muqawama ndio njia pekee ya kukabiliana na adui na kuongeza kuwa: "Mapambano ni njia pekee ya kupata ushindi mbele ya sera za Marekani, na ushindi wa taifa la Iran uko karibu."

Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyasema hayo Jumanne na kuongeza kuwa sera za Marekani duniani zimegonga mwamba na kuongeza kuwa: "Leo Iran ina nguvu na uwezo kubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote na inapambana na maadui na mapambano hayo yanatokana na utumbulisho wa Kiislamu na kimapinduzi na kitaifa wa wananchi Waislamu wa Iran."

Kamanda wa IRGC ameendelea kusema kuwa, hivi sasa Wamarekani wanakabiliwa na ukosefu wa stratijia na kuongeza kuwa: "Maadui wa Iran wamechoka na hivi sasa zama za Marekani zinakaribia kufika ukingoni."

Mapambano na muqawama ni chaguo la dhahabu na amilifu kwa taifa la Iran katika kipindi cha miaka 40 iliyopita. Baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, maadui wa taifa la Iran hasa Marekani wametekeleza kila aina ya njama ili kuzuia ustawi wa taifa la Iran na kwa dhana yao potovu, wapate kuifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iwe nchi tegemezi. Lakini pamoja na hayo, mapambano yenye lengo na erevu ya taifa la Iran yameweza kusambaratisha njama hizo za Marekani.

Utambulisho wa Kihistoria, Kiislamu na Kimapinduzi wa taifa la Iran hauwezi kuruhusu taifa hili liangamie. Utambulisho wa kutaka uhuru na kujitegemea ambao ulidhihirika wazi baada ya kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu ulipelekea Jamhuri ya Kiislamu kuibuka kama nchi huru, yenye kujitegemea na yenye uwezo mkubwa kieneo na duniani.

Historia ya miaka 40 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu imejaa uzoefu wa mapambano yalipopata ushindi ambapo miaka minane ya kujihami kutakatifu (wakati wa vita vya utawala wa Baath wa Saddam dhidi ya Iran) ni mfano mzuri wa mapambano ya taifa la Iran mbele ya wavamizi.

Hivi sasa pia,  Marekani imeanzisha vita vya kiuchumi dhidi ya taifa la Iran lakini mapambano ya aina yake ya taifa la Iran yamevuruga mahesabu ya watawala wa Marekani.

Rais Donald Trump wa Marekani anaonekana kuwapita marais wote waliotangulia wa nchi hiyo katika uhasama dhidi ya taifa la Iran kwani anatekeleza 'vitisho na mashinikizo ya juu zaidi' dhidi ya taifa la Iran.

'Muqawama na mapambano ya juu zaidi na athirifu' ya taifa la Iran mbele ya sera za 'vitisho na mashinikizo ya juu zaidi' ya Marekani, ni jambo ambalo limewachanganya na kuwakasirisha sana wakuu wa White House.

Marekani imepata pigo kiasi kwamba, sasa nchi hiyo inajaribu kueneza hadaa na kuwasilisha ushahidi bandia ili kuiarifisha Iran kama nchi inayovuruga usalama wa eneo lakini pia katika hili imefeli kwani hakuna anayeamini madai yake hayo duniani.

Kuhusiana na hili, Mark Dankof  mwanaharakati wa kisiasa wa chama tawala cha Republican nchini Marekani  amesema madai ya wakuu wa Marekani kuhusu kuhusika Iran katika hujuma dhidi ya meli za mafuta katika Bahari ya Oman ni kukaririwa madai ya hadaa ya kihistoria ya serikali za Marekani kwa ajili ya kuanzisha vita. Ameongeza kuwa: "Ili kuituhumu Iran wanaibua nyaraka bandia."

Gazeti la Kimarekani la Washington Post limeandika: "Tuhuma za Rais Donald Trump dhidi ya Iran kuhusu hujuma dhidi ya meli mbili hazijaweza kutiliwa maanani kutokana na kuwa hazina itibari na ni urongo mtupu."

Sera za msingi na mapambano yaliyozaa matunda ya taifa la Iran yametokana na utambulisho wa Kiislamu na kimapinduzi wa taifa hili na kwa msingi huo watawala wa Marekani hawajaweza kufikia ndoto yao kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kushindwa uhasama wa hivi sasa wa Marekani ni ukurasa mwingine katika historia ya uhasama wa watawala wa Marekani dhidi ya taifa shupavu la Iran. 

Madai yasiyo na msingi ya Trump, hasa madai yake ya kulivunjia heshima taifa la Iran kwa kulitaja kuwa eti ni taifa la kigaidi ni sehemu ya uhasama huo. Lakini sasa imewabainikia wazi wote kuhusu nani magaidi halisi. Leo kuna nyaraka zenye ushahidi wa wazi ambao unaonyesha kuwa, watawala wa Marekani na waitifaki wao katika eneo la Asia Magharibi ndio magaidi halisi.



/129