20 Julai 2019 - 07:47
Israel yatiwa kiwewe na nguvu za kijeshi za Hizbullah ya Lebanon

Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni wa Israel vimetangaza habari ya kuchukuliwa hatua mpya na utawala huo ghasibu za kuimarisha ulinzi katika maeneo ya kiistratijia katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni kutokana na kuiogopa Harakati ya Mapambanao ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

(ABNA24.com) Vyombo hivyo vya habari vya Kizayuni likiwemo gazeti la Haaretz jana vilifichua kuwa, baada ya Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon kutoa maelezo kuwa Israel ina vituo 20 vya kiistratijia kama vile shirika la umeme na mabomba ya gesi na kwamba kama utawala wa Kizayuni utaanzisha vita vipya basi maeneo hayo hayatobaki salama, viongozi wa Israel wameingia woga na kuamua kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo.

Katika hotuba yake ya hivi karibuni aliyoitoa kwa mnasaba wa kukumbuka vita vya siku 33 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah alisema kuwa, muqawama umepiga hatua kubwa za ulinzi wa makombora na wa ndege zisizo na rubani na kusisitiza kuwa, hivi sasa muqawama una nguvu kubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote na viongozi wa Israel wanauogopa zaidi hivi sasa muqawama kuliko wakati wowote ule.

Hivi karibuni makundi ya muqawama ya Palestina yalitoa majibu makali kwa uvamizi wa utawala wa Kizayuni huko Ghaza na kuilazimisha Israel ikomeshe uvamizi wake huo muda mchache tu tangu ilipouanzisha.


/129