22 Julai 2019 - 06:08
Ujumbe wa Putin kwa Bashar al Assad: Russia itaendelea kuiunga mkono Syria

Rais wa Russia amesisitiza katika ujumbe aliomtumia Rais mwenzake wa Syria kwamba Moscow itaendelea kuunga mkono umoja wa ardhi yote ya Syria.

(ABNA24.com) Rais Vladimir Putin wa Russia alisema jana Jumapili katika ujumbe aliomtumia Rais Bashar al Assad wa Syria kwa mnasaba wa kutimia miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi mbili hizo kuwa: Russia itaendelea kuunga mkono mamlaka na umoja wa ardhi yote ya Syria. Putin amesisitiza kuwa Russia na Syria zina mtazamo wa pamoja kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi na misimamo mikali na akasema nchi mbili hizo zinaboresha uhusiano wao katika fremu ya kuimarisha amani na uthabiti katika eneo na ulimwenguni kwa ujumla.

Rais wa Russia ametoa hakikisho hili kwamba magaidi waliopo katika ardhi ya Syria hatimaye watashindwa kwa jitihada za pamoja za nchi mbili hizo. Rais Putin amesema anataraji kuwa wananchi wa Syria karibuni hivi watarejea katika maisha ya amani na utulivu. Vita vya ndani vilianza Syria mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi likiwemo kundi la kitakfiri la Daesh na Jabhatul Nusra kuanza kutekeleza mashambulio makubwa kwa uungaji mkono wa nchi za Magharibi lengo likiwa ni kuipindua serikali halali ya Rais Bashar al Assad.  

Damascus mwaka 2018 ilifanikiwa kutoa kipigo kikali kwa makundi ya kigaidi kwa kushirikiaa na Iran na Russia; na kukomboa pia akthari ya maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na makundi hayo ya kigaidi.



/129

X