(ABNA24.com) Qais al Khazali amesema kuwa kufanyika uchaguzi wa kabla ya wakati hakutaiepusha Iraq na hali ya sasa iliyonayo. Al Khazali ameongeza kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Adel Abdulmahdi si chanzo kikuu cha mgogoro wa nchi hiyo na akasema wafanya maandamano waendelee kusalia katika maidani za miji ya nchi hiyo hadi hapo matakwa yao yatakapopatiwa ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Asaeb Ahl al Haq amesisitiza kuwa upande wa tatu kwenye maandamano hayo unatekeleza mauaji dhidi ya waandamanaji na askari usalama; jambo ambalo linapasa kuchunguzwa ili kuwatambua wahusika wa mauaji hayo.

Baadhi ya miji ya Iraq katika wiki za karibuni imekumbwa na maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali ngumu ya maisha, huduma mbovu kwa umma, ukosefu wa ajira na ufisadi serikalini, hata hivyo maandamano hayo hivi karibuni yameingiliwa na pande za nchi ajinabi na hivyo kuibua machafuko. Hadi sasa mamia ya watu wameuawa na kujeruhiwa katika machafuko hayo.
.........
340