-
Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom ametembelea Shirika la Habari la ABNA | Ayatollah Faqihi amesisitiza umuhimu wa uaminifu katika Habari
Akiashiria umuhimu wa ukweli na uaminifu katika vyombo vya habari, Ayatollah Faqihi alisema: "Ikiwa tutadumisha ukweli na uaminifu katika uwanja wa taarifa na usambazaji wa habari, basi kwa hakika tunaweza kutoa huduma kubwa katika uwanja huu."
-
Ni kwa namna ipi Sala hukataza maovu?
Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema ndani ya Qur'an Tukufu anasema: (اتْلُ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِنَ الْكِتَابِ وَأَقِمِ الصَّلَاةَ ۖ إِنَّ الصَّلَاةَ تَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ ۗ وَلَذِكْرُ اللَّهِ أَكْبَرُ ۗ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَصْنَعُونَ). "Soma uliyo funuliwa katika Kitabu, na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yatenda".
-
Habari Pichani | Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Biteko awapongeza Walimu wa Al-Muntadhir kwa Malezi ya Watoto
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlu-Bayt (a.s) - ABNA - Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Biteko awapongeza Walimu wa Al-Muntadhir kwa Malezi ya Watoto katika mkusanyiko mkubwa wa watu uliofanyika leo hii katika viwanja vya Shule ya Al-Muntadhir ili kuadhimisha Siku ya Usonji Duniani. Mkusanyiko huo ulikuwa na lengo la kuwambia walimwengu kuwa Watanzania tunambua na kujali watoto wenye mahitaji maalum. Naibu Waziri amesema: Shule za Al-Muntadhir zimeanza na sisi washiriki tuna wajibu wa kuendeleza na kuenzi azma hii.
-
Waisraeli waandamana kupinga kuanza tena vita vya Gaza
Maelfu ya waandamanaji wamejitokeza katika mitaa ya Tel Aviv kushiriki katika maandamano mapya ya kupinga serikali ya utawala haramu wa Israel, wakati ambapo Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu alipokutana na Rais wa Marekani, Donald Trump mjini Washington.
-
Msemaji wa Taliban: Askari wa Marekani hawawezi kuruhusiwa kuwepo ndani ya ardhi ya Afghanistan
Msemaji wa serikali ya muda ya Afghanistan amesisitiza kuwa haiwezekani askari wa Marekani waruhusiwe kwenda na kuwepo ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
-
Mashirika sita ya UN: Vita vya Ghaza ni ishara ya kutojaliwa hata chembe maisha ya binadamu
Wakuu wa mashirika sita ya Umoja wa Mataifa wametoa indhari kali kuhusu hali ya Ukanda wa Ghaza na kutaka usitishaji vita utekelezwe tena na kwa haraka sana, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya katika eneo hilo linaloendelea kuandamwa na mashambulio ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Ndege za kivita za Marekani zashambulia Yemen karibu mara 30 katika muda wa chini ya siku moja
Marekani imefanya karibu mashambulizi 30 ya anga katika majimbo kadhaa kote nchini Yemen katika muda wa chini ya siku moja, na kushadidisha uchokozi wake dhidi ya taifa hilo, katika kile ambacho wataalamu wamekitaja kuwa ni harakati za kujishinda yenyewe za kusitisha bila mafanikio operesheni za Sana'a zinazotekelezwa dhidi ya Israel na waungaji mkono wake kwa ajilii ya kuwatetea wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Pezeshkian: Wamarekani wathibitishe kivitendo kuwa kweli wanataka mazungumzo
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa, viongozi wa Marekani wana wajibu wa kuthibitisha kivitendo kuwa kweli wanataka mazungumzo na Tehran.
-
Araghchi: Iran, US zitafanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja Oman
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu na Marekani zitafanya "mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya ngazi ya juu" nchini Oman karibuni hivi.
-
Wanamitandao wa Iran: "Trump anasema uwongo", "Marekani Shetani hatoki hatiani kwa mazungumzo"
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wametuma jumbe mbalimbali za kukosoa sera za Rais wa Marekani dhidi ya Iran na ushirikiano wake na viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika kufanya jinai za kivita huko Ghaza.
-
Hitilafu za viongozi wa Ulaya kuhusu jibu la vita vya ushuru vya Trump
Tangazo la kutoza ushuru mpya la Rais wa Marekani, Donald Trump, dhidi ya nchi 180 duniani, zikiwemo nchi za Umoja wa Ulaya, limeibua hisia tofauti kutoka kwa nchi mbalimbali duniani.
-
Ushuru wa Trump; Masoko ya hisa ya US yazidi kuporomoka
Hisa za Marekani zimeendelea kuporomoka kwa siku ya tatu mfululizo, huku mashirika na wawekezaji wakishindwa kuelewa malengo ya mipango mipya ya ushuru ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
-
Maandamano ya kumpinga Trump yamesababishwa na mambo mengi
Huku wananchi wa Marekani wakiendelea kukasirishwa na siasa za kidikteta na uingiliaji kati za Trump, Elon Musk na serikali yao, wataalamu wanasema kuna sababu nyingi zilizopelekea mamia ya maelfu ya watu wajitokeze kote Marekani na nje ya Marekani kupinga siasa za Washington.
-
China yaapa 'kupambana hadi mwisho' dhidi ya ushuru wa Trump
Wizara ya Biashara ya China imeionya Marekani dhidi ya kuingia katika msururu wa vikwazo vya kibiashara vya 'kujibishana mapigo' baada ya rais wa nchi hiyo Donald Trump kutishia kuweka ushuru wa ziada kwa bidhaa za China zinazoingizwa nchini Marekani.
-
Mwanaume Mkristo aliyesilimu kwa sababu ya tabia nzuri ya Ali (AS)
Je, Hadhrat Ali (AS) alifanya nini wakati Mwanaume mmoja Mkristo aliposilimu? Kwa heshima ya kusilimu kwake, alimpa ngao yake (inayovaliwa vitani) na kumpa nafasi katika Serikali.
-
Ripoti ya Picha | Mashia nchini Ujerumani wakiomboleza katika kumbukumbu ya kuharibiwa kwa Makaburi ya Maimamu wa al-Baqi (a.s)
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (as) - ABNA -, Marasimu za Maombolezo ya kumbukumbu ya kuharibiwa Makaburi ya Maimamu waliozikwa katika ardhi Tukufu ya Baqi' - Madina (Amani iwe juu yao) zilifanyika kwa kuhudhuriwa na kundi la wapenzi na wafuasi wa Ahlul Bayt wa isma na utoharifu (AS) katika Maukib ya "Abis Al-Sha'kiri" katika Mji wa Cologne, Ujerumani.
-
Ripoti ya Picha | Maandamano huko Ramallah dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) - ABNA - Kumefanyika maandamano makubwa katika Mji wa Ramallah katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa kushirikisha idadi kubwa ya Wapalestina, kulaani jinai na hujuma zinazoendelea kufanywa na jeshi la Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Wito wa Maandamano kufuatia Mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni
Kufuatia mashambulio hayo ya kinyama ya utawala wa Kizayuni, Baraza la Uratibu wa Tabligh za Kiislamu limetoa taarifa likiwaalika Wananchi Watukufu wa Tehran kushiriki katika maandamano yatakayofanyika kesho katika Medani ya Palestina.
-
Safari ya Netanyahu kuelekea Marekani imeisha kwa kasi isiyo ya kawaida!
Chombo cha Habari cha Kiebrania kilifichua sababu iliyomfanya Waziri Mkuu wa Israel kuitwa katika Ikulu ya White House kukutana na Rais wa Marekani.