-
Mgogoro unaoshadidi wa Chuki dhidi ya Uislamu barani Ulaya
Baada ya kuanza vita vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza, ripoti zinaonesha ongezeko la asilimia 140 ya uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu katika nchi za Ulaya, hasa Ujerumani — jambo ambalo limegeuka kuwa tishio kubwa kwa jamii za Ulaya.
-
Zakharova:Tunasubiri kwa hamu safari ya ujumbe wa Iran mjini Moscow
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema kuwa nchi hiyo inasubiri kwa hamu ziara ya ujumbe wa Iran mjini Moscow ili kukutana na kuzungumza na wenzao wa Russia.
-
Hamas: Madai ya adui kuhusu hospitali ya Al Mamadani ni uongo unaorudiwa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa tamko kujibu madai ya uongo ya jeshi katili la adui Israel kuhusu kuripuliwa hospitali ya Baptist huko Gaza, na kuyataja madai hayo kuwa ni "uongo unaorudiwa" wa kujaribu kuhalalisha jinai za kivita za utawala ghasibu wa Kizayuni.
-
Jeshi la Yemen laangusha ndege ya 19 ya kivita ya Marekani
Jeshi la Yemen limetangaza kuangusha tena ndege ya kisasa ya kivita isiyo na rubani aina ya MQ-9 ya Jeshi la Marekani katika anga ya nchi hiyo.
-
Abu Ubaidah: Wapalestina hawatosahau Wayemen walivyosimama nao bega kwa bega
Msemaji wa Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, Wapalestina hawatosahau namna Wayemen walivyosimama imara na bega kwa bega pamoja nao katika Jihadi ya kuikomboa ardhi ya Palestina.
-
Jinai za kinyama za Israel Ghaza hazina udhibiti, Wapalestina wengine 37 wauawa shahidi
Mashambulio makubwa na ya kinyama yaliyofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika maeneo mbalimbali ya Ghaza yamewaua shahidi Wapalestina wengine wasiopungua 37.
-
Kushindwa mhimili wa vita wa Kizayuni na Marekani katika vita huko Yemen na Gaza
Licha ya mashambulizi yanayoendelea kufanywa na mhimili wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Yemen na Gaza, bado vikosi vya jeshi la Yemen na Muqawama wa Palestina vinaendelea kukabiliana na wavamizi hao.
-
Iraq yaonya dhidi ya kuibuka upya ISIS nchini Syria
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq, Fuad Hussein ameonya kuhusu kushadidi harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika nchi jirani ya Syria, kufuatia kuanguka kwa serikali ya Rais Bashar al-Assad mwishoni mwa mwaka jana.
-
Mawaziri wa mambo ya nje wa Misri na Kuwait wakaribisha mazungumzo kati ya Iran na Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Abbas Araghchi amezungumza na mawaziri wenzake wa Misri na Kuwait na kuwaeleza kuhusu msimamo wa Tehran juu ya mazungumzo yasiyo ya ana kwa ana iliyofanya na Marekani.
-
Kazem Gharib Abadi: Rafael Grossi kuwasili Tehran Jumatano
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa ametangaza kuwa, Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atiomiki (IAEA) atawasili Tehran Jumatano wiki hii na atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran.
-
Habari Pichani | Dr.Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (S), Dar-es-Salam, akiwa katika Mkutano wa Ukaribu na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Dr. Ali Taqavi, Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (S), Dar-es-Salam - Tanzania, akiwa katika Mkutano wa Ukaribu baina yake na Mh.Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt. Abubakary Zubeiry bin Ally, na baadhi ya Maulamaa na Wanachuoni wa Shia na Sunni nchini Tanzania. Imam Ja'far Sadiq (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), alimuuliza Fudhail swali hili kwamba: "«تَجْلِسُونَ وَتَتَحَدَّثُونَ؟» " / Je! Mnakaa na Mnazungumza?. Fudhail akasema: Ndio. Imam Sadiq (a.s) akasema: Kwa hakika napenda vikao kama hivyo.
-
Habari Pichani | Mkutano wa Kisayansi kwa anuani hii: " Umoja wa Waislamu Katika Kivuli cha Quds" - Jamiat al-Mustafa (S), Dar-es-Salam - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Siku ya Al-Quds ni wakati ambao tunapaswa kuwaonya Mataifa ya Uistikbari Ulimwenguni dhidi ya Palestina na Wanadamu wote wanaodhulumiwa, na wenye nia ya kuwadhibiti Waislamu na Uislamu na kuutokomeza kabisa, ya kwamba Uislamu hautadhibitiwa tena na nyinyi kupitia mawakala wenu waovu na wamwagaji damu katika eneo la Mashariki ya Kati. Jamiat Al-Mustafa (S), Dar -es-Salam - Tanzania, inaichukulia Kila Siku ipitayo kuwa ni Siku muhimu kwa ajili ya Quds, bali inafaa Kila Siku kuitwa kuwa ni Siku ya Quds. Katika muktadha huu, Jamiat al-Mustafa (S), Dar-es-Salam - Tanzania", chini ya Kiongozi wake Mkuu Hojjat Al-Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, ilifanikiwa kuratibu Mkutano wa Kisayansi kwa anuani hii:"Umoja wa Waislamu Katika Kivuli cha Quds".
-
Habari Pichani | Harakati za Kielimu za Hawzat Imam Ridha (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya "Hojjatul Asr Society of Tanzania" -Ikwiriri- Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Hawzah Imam Ridha (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya "Hojjatul Asr Society of Tanzania", Ikwiriri - Tanzania, inayoongozwa na Maulana Samahat Sayyid Arif Naqavi (H.A) inaendelea na harakati zake za kielimu katika madarasa mbalimbali ya Hawzah hii. Maulana Samahat Sayyid Arif Naqavi, Kiongozi Mkuu wa Taasisi hii, amefanya ziara muhimu katika vituo mbalimbali vya Kidini vya Taasisi hii ikiwe Hawzah hii ya Imam Ridha (a.s). Elimu ni Nuru, na Ujahili ni Giza.
-
Habari Picha + Video | Wanafunzi wa Hawzah ya Hazrat Zainab (sa) wakijishughulisha na Kilimo / Kilimo ni UTI wa Mgongo wa Uchumi wetu
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mabanati wa Hawzah ya Hazrat Zainab (amani iwe juu yake), wakiwa katika hali ya kujishughulisha na kazi ya Kilimo. Kila mmoja wao katika kundi la watu watatu, anamiliki kipande cha ardhi. Wanalima na kupanda mazao yao, na wakati wa kuvuna, sisi (Uongozi wa Jamiat Al-Mustafa - Dar-es-salaam, Tanzania) tunanunua mavuno / bidhaa hizo kutoka kwao. Kilimo ni UTI wa Mgongo wa Uchumi wetu. Hivyo tufikiri zaidi na kuwaza katika Kilimo. Tujaribu kufanya Kilimo hata kwa kiasi kidogo.
-
Sikiliza Utamu wa Qur'an Tukufu! | Kwa Hakika Qur'an Tukufu ni Tabibu Mkuu wa Nyoyo + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sikiliza utamu wa sauti inayokariri Kurani Tukufu! Hakika Qur'an Tukufu ni Tabibu Mkuu wa Nyoyo.
-
Habari Pichani | Huduma za Kijamii za Taasisi ya Darul - Muslimina, Dodoma Tanzania zilivyokuwa ndani Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ya Mwaka huu 1446H
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ya Mwaka huu 1446H, Taasisi ya Darul Muslimeen - Dodoma Tanzania, ilijihusisha na utoaji wa Huduma mbalimbali za kijami. Miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na kupata heshima ya kusambaza vyakula vya Iftar na Daku kwa Madrasa mbalimbali za Kiislamu na vituo vya Bweni vya Wanafunzi wa Kidini, vinavyopatikana katika viunga vya Mji wa Dodoma, Tanzania.
-
Ripoti Katika Picha | Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Qur'an na Hadithi - Dar-es-salaam, Tanzania limefanyika kwa mafanikio makubwa
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tamasha hili limefanyika kwa mafanikio makubwa chini ya Uongozi na Usimamizi wa Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa, Dar-es-salaam - Tanzania - Dr. Ali Taqavi.