Abu Ubaidah, amebainisha kuwa, wananchi wa Yemen wamelipa gharama kubwa ya kuhimili maafa makubwa yanayowafika kwa kujitolea kwao kwa ajili ya Palestina, lakini wangali wamesimama imara na kushikamana na msimamo wao wa kuwa bega kwa bega na Ghaza, jambo ambalo wananchi wa Palestina hawatalisahau katu.
Msemaji wa Al-Qassam amesisitiza kwa kusema: "licha ya kulipa gharama kubwa kwa damu zao zenye thamani kubwa na rasilimali za nchi yao, kwa kujitolea kwa ajili ya Palestina na Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, ndugu zetu wa kweli wa Yemen wangali wanaendelea kuupoozesha moyo wa utawala wa Kizayuni kwa kutangaza kuwa wataendelea kusimama imara na bega kwa bega na Ghaza inayoandamwa na vita angamizi vya mauaji ya kimbari".
Abu Ubaidah ameongezea kwa kusema: Palestina na watu wake hawatausahau msimamo huo wa heshima na sharafu wa watu wa Yemen wanaosimama nao bega kwa bega, pamoja na irada hiyo thabiti inayotoa bishara ya kheri kwa umma huu na uwezo ulionao wa kuvuruga usalama wa utawala huo wa Kizayuni.
Awali kabla ya tamko hilo la msemaji wa Al-Qassam, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilitangaza rasmi kuwa makombora mawili yamerushwa kutoka Yemen kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) na kwamba juhudi za kuyazuia zinaendelea.
Jana Jumapili, kanali ya 14 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni iliripoti kuwa, jeshi la utawala huo linafuatilia kutungua kombora lililorushwa kutoka Yemen kuelekea katikati mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.
Duru za habari za Kiebrania zimetangaza kuwa makombora matatu ya ulinzi wa anga yalirushwa kukabiliana na shambulio hilo na kwamba ving'ora vya hali ya hatari vilisikika katika baadhi ya maeneo ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.../
342/
Your Comment