Katika kufanikisha njama yake ya kuangamiza kizazi cha Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza, utawala wa Kizayuni sasa hivi unaendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa ukanda huo mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa na uungaji mkono wa kila hali wa Marekani.
Duru za Palestina zimetangaza kuwa raia wasiopungua watatu wameuawa shahidi katika mashambulizi ya leo yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni kwenye kitongoji cha Shuja'iya mashariki mwa Ghaza.
Wakati huo huo, jeshi la utawala wa Kizayuni limetoa amri mpya ya kuwataka Wapalestina wanaoishi Khan Yunis waondoke katika mji huo na kuelekea kusini mwa eneo la Al-Mawasi.
Wizara ya Afya ya Ghaza imetoa taarifa ikisema: "katika ukatili wa kinyama wa leo wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza, hadi sasa imethibitishwa kuwa raia wasiopungua 37 wameuawa shahidi".
Kwa uchache Wapalestina 25 ya 37 waliokufa shahidi wameuawa katika mashambulio yaliyofanywa na jeshi la Kizayuni katikati na kusini mwa ukanda huo.
Pamoja na hayo, kutokana na uharibifu mkubwa uliofanywa na jeshi la utawala ghasibu wa Israel na kubakia miili mingi iliyoachwa chini ya vifusi, idadi halisi ya Mashahidi na majeruhi wa ukatili wa kinyama wa Wazayuni ni kubwa zaidi kuliko takwimu za awali zilizotangazwa na duru za Palestina.../
342/
Your Comment