Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

27 Oktoba 2022

17:30:22
1317827

Magaidi 17 wa al-Shabaab wauwa katika operesheni mpya Somalia

Vyombo vya intelejensia vya Somalia vikishirikiana na vya kimataifa vimeangamiza wanachama 17 wa kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Kwa mujibu wa Wizara ya Habari ya Somalia, magaidi hao waliuawa katika operesheni ya usiku wa kuamkia jana katika mji wa Hawadley, yapata kilomita 40 kaskazini mwa Mogadishu.

Taarifa ya wizara hiyo imesema: Operesheni hiyo ilifanywa na Idara ya Taifa ya Intelijensia kwa ushirikiano na washirika wa kimataifa. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, wanachama hao wa al-Shabaab walishambuliwa walipokuwa wamekusanyika katika eneo moja mjini Hawadley, ambapo 17 miongoni mwao wameuawa.

Habari zaidi zinasema kuwa, makanda waandamizi wa al-Shabaab na magenge mengine yenye mfungamano na al-Qaeda wameangamizwa kwenye operesheni hiyo.

Vyombo vya usalama vya Somalia vimeshadidisha operesheni za kupambana na magenge ya kigaidi katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Taarifa ya Wizara ya Habari ya Somalia imesema kufikia sasa magaidi 150 wameuawa katika operesheni za hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, raia 1,242 wameuawa katika mashambulizi ya kigaidi nchini Somalia baina yam waka 2018 na 2019, mbali na 1,735 kujeruhiwa.

342/