Main Title

source : Parstoday
Jumanne

15 Novemba 2022

16:44:48
1323363

Utawala wa Kizayuni; kizuizi kikuu cha uwepo wa Asia Magharibi pasina silaha za maangamizi ya umati

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameutaja utawala wa Kizayuni kuwa kizuizi kikuu cha uwepo wa Asia Magharibi isiyokuwa na silaha za maangamizi ya umati.

Utawala wa Kizayuni ambao unamiliki silaha za nyuklia ambapo kwa mujibu wa ripoti nyingi za kuaminika hivi sasa unamiliki vichwa vya nyuklia kati ya 200 hadi 400, umekataa katakata kujiunga na Mkataba wa NPT unaopiga marufuku usambazaji wa silaha za nyuklia.

Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema katika kikao cha 3 cha Mkutano wa Asia Magharibi Pasina Silaha za Nyuklia kwamba: kupendekeza masuala yasiyo na weledi na yasiyo sahihi kuhusu masuala ya nyuklia ya Iran si tu hakutawasaidia wale wanaotoa madai hayo bali kutaweka mbali suala la kuzingatiwa tishio kuu la kuwa na eneo la Asia Magharibi lislo na silaha za maangamizi ya umati ambalo ni utawala wa Kizayuni.

Balozi Iravani amebainisha mitazamo na maoni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kuashiria uanachama wa Tehran katika miundo ya kimataifa kuhusu silaha za maangamii ya halaiki na kusisitiza kuhusu sera endelevu za Iran juu ya kuangamizwa kikamilifu silaha hizo za maangamizi ya umati ikiwemo pia mpango rasmi uliopendekezwa mwaka 1974 wa kuwa na eneo salama pasina silaha za maangamizi ya halaiki katika Asia Magharibi. 

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, anataraji kuwa nchi nyingine wanachama wa NPT zitapasisha sera madhubuti kama hizo na kuacha kufuata kibubusa kila sera zinazokwamisha kuasisiwa eneo kama hilo. 

342/