Main Title

source : Parstoday
Jumatano

16 Novemba 2022

17:20:26
1323742

China yapinga kutimuliwa Russia katika jumuiya ya nchi zinazounda G20

Waziri wa mambo ya nje wa China amesema anaunga mkono mchango wa Russia katika G20 na akasisitiza kuwa hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuinyima Moscow nafasi ya kushiriki katika jumuiya za pande kadhaa.

Kikako cha siku mbili cha viongozi wa nchi zinazounda kundi la G20 kilianza jana Jumanne katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia huku zikiwepo tofauti na mivutano mikali kati ya nchi wanachama kuhusu operesheni za kijeshi za Russia ndani ya Ukraine, nishati na usalama wa chakula duniani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la RIA Novosti, waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ametoa kauli hiyo katika mazungumzo aliyofanya pembeni ya kikao hicho na mwenzake wa Russia Sergey Lavrov na akaongezea kwa kusema: Sisi tunaunga mkono mchango wenye thamani wa Russia katika kundi hili na jumuiya zingine za kimataifa na tunaitakidi kuwa hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kuinyima Moscow haki hii ya kimantiki na ushirikiano inatoa katika jumuia za pande kadhaa.

Kinyume na miaka iliyopita, kikao cha mwaka huu cha viongozi wa nchi zinazounda G20 kimeanza bila ya picha ya pamoja wanayopiga viongozi, kutokana na tofauti na mivutano iliyopo baina ya nchi wanachama.

Tokea awali, maafisa wa Indonesia walikuwa wameshatangaza kwamba katika kikao cha mwaka huu hakutakuwepo na hafla ya upigaji picha yoyote ya pamoja, hatua ambayo haijawahi kuchukuliwa katika historia ya kundi la G20.

Kwa kawaida, na kulingana na desturi waliyojiwekea kila mwaka, viongozi wa G20 huwa wanapiga picha ya pamoja kabla ya kuanza kikao chao rasmi.

Katika kikao cha mawaziri wa mambo ya nje pia, waziri wa mambo ya nje wa Indonesia alitangaza kuwa upigaji picha ya pamoja umefutwa kutokana na wanadiplomasia wa Magharibi kupinga kuhudhuria waziri wa mambo ya nje wa Russia katika kikao cha wanachama.../

342/