Main Title

source : Parstoday
Jumatano

31 Mei 2023

13:57:39
1370145

Ndege ya abiria iliyoundwa Iran yafanyiwa majaribio kwa mafanikio

Ndege ya abiria na mizigo ya iliyopewa jina la Simorgh imeundwa kikamilifu na wataalamu wa Shirika la Viwanda vya Anga la Wizara ya Ulinzi ya Iran na imefanyiwa majaribio ya kuruka kwa mafanikio makubwa.

Kwa mujibu wa taarifa, ndege ya abiria na mizigo ya Simorgh ni ndege ya kisasa kabisa ambayo inafaa kukidhi mahitaji ya vitengo vya kijeshi na kiraia  nchini Iran. Aidha imeundwa kwa kuzingatia hali ya hewa ya Iran na kwa mujibu wa viwango na kanuni za kimataifa.

Wepesi, uwezo wa kubeba mizigo, kufaa hali ya hewa ya nchi, uwezo wa kutua na kuruka katika njia fupi za ndege, wepesi na kasi ya ndege hii katika kutoa huduma za haraka kama vile ambulensi ni miongoni mwa sifa na matumizi ya "Simorgh" .
Uundaji wa ndege hii umeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha nyingi za kigeni  na kuongeza ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa vijana Wairani. 

Aidha ndege hii ni kielelezo cha itikadi ya uchumi wa kimuqawama au kimapambano katika Wizara ya Ulinzi, ustawi wa juu wa kiteknolojia na viwanda na hatimaye ujumuishaji wa uwezo wa kitaifa wa kuunda bidhaa za teknolojia ya hali ya juu katika anga.

Brigedia Jenerali  Mohammad Reza Qaraei Ashtiani, Waziri wa Ulinzi wa Iran akizungumza mbele ya maafisa wa ngazi za juu jeshini amepongeza mafanikio hayo ya kitaifa.

Amesema Viwanda vya Ulinzi vya Iran vmeunda meli ya kivita ya Dana ambayo hivi karibuni ilizunguka dunia kwa muda wa miezi minane. Aidha amesema Viwanda vya Ulinzi vya Iran karibuni hivi vilizindua kombora la kimkakati la Khorramshahr 4 na sasa kumepatikana mafanikio ya majaribio yaliyofana ya ndege ya abiria na mizigo ya  Simorgh. 

342/