Amir-Abdollahian aliyasema hayo katika mahojiano na gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Figaro, lililochapishwa Jumatatu, kuhusiana na kurejeshwa kwa uhusiano kati ya nchi hizi mbili.
"Amesema katika sera ya mambo ya nje ya serikali ya sasa ya Iran, uhusiano na majirani zetu ni kipaumbele," na kuongeza kwamba hii ndiyo sababu Jamhuri ya Kiislamu ilifanya mazungumzo ya usalama na Saudia kwa miezi kadhaa huko Baghdad na Oman.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameendelea kusema kwamba hatimaye wakati wa ziara ya rais wa China nchini Saudi Arabia, pendekezo imara liliwekwa mezani.
Ameongeza kuwa matokeo yake yalikuwa upatanishi wa China ambao ulifanya iwezekane kuchukua hatua madhubuti kati ya Tehran na Riyadh.
Mnamo Machi 10, baada ya siku kadhaa za mazungumzo mazito yaliyoandaliwa na China, hatimaye Iran, na Saudi Arabia zilikubali kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na kufungua tena balozi zao miaka saba baada ya uhusiano kukatika.
Katika taarifa ya pamoja baada ya kusaini makubaliano hayo, Tehran na Riyadh zimesisitiza haja ya kuheshimu mamlaka ya kitaifa ya kila mmoja na kujiepusha na kuingilia masuala ya ndani ya upande wa pili.
Nchi mbili ziliafiki kutekeleza makubaliano ya ushirikiano wa kiusalama yaliyotiwa saini Aprili 2001 na makubaliano mengine yaliyofikiwa Mei 1998 ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kibiashara, uwekezaji, kiufundi, kisayansi, kitamaduni, michezo na masuala ya vijana.
Kwingineko katika matamshi yake, Amir-Abdollahian amebainisha kuwa serikali ya Saudia imefanya uwekezaji nchini Iran kuwa kipaumbele.
342/