Main Title

source : Parstoday
Jumatano

31 Mei 2023

13:59:27
1370148

Kan'ani aliambia Bunge la Ulaya: Haki za binadamu zina uhusiano gani na kuwaunga mkono magaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amezungumzia suala la kualikwa kiongozi wa kundi la kigaidi la MKO katika Bunge la Ulaya na nara zinazotolewa na nchi za Ulaya kuhusu haki za binadamu na kuhoji: Haki za binadamu zina uhusiano gani na kuwaunga mkono magaidi?

Bunge la Ulaya hivi karibuni lilikuwa mwenyeji wa kiongozi wa kundi la kigaidi la MKO.

Akijibu hatua ya Bunge la Ulaya ya kumkaribisha bungeni kiongozi wa kundi la kigaidi la MKO, Nasser Kan'ani Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Kinyume na nara za haki za binadamu zinazotolewa na Bunge la Ulaya inasikitisha kuona kwamba baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zinafumbia macho rekodi  nyeusi ya wale wote waliohusika na mauaji ya zaidi ya watu elfu 17 wakiwemo watoto, wanawake, wanaume, viongozi na wawakilishi wa wananchi wa Iran katika Bunge na kisha zinamkaribisha kiongozi wa kundi la kigaidi. 

Kanani Chafi amehoji kwamba: Haki za binadamu zina uhusiano gani na kuwaunga mkono magaidi?!

Mwezi Machi mwaka huu pia Bob Blackman mbunge wa Uingereza ambaye pia ni Mkuu wa Kundi la Urafiki wa Mabunge ya Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel alieleza jinsi alivyokutana na viongozi wa kundi la kigaidi la MKO huko Albania na  kumtaja mkuu wa kundi hilo la kigaidi kuwa rais wa aliyechaguliwa na eti baraza la kitaifa la Iran. 

Kuhusiana na suala hilo, Sayyid Mehdi Hosseini Matin balozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu mjini London alituma ujumbe katika ukurasa wake wa Twitter akijibu Twitter ya mbunge wa Uingereza ambaye hivi karibuni alitembelea kambi ya kundi la kigaidi la MKO huko Albania na kusema: Kitendo cha kukutana na adui anayechukiwa zaidi wa taifa la Iran kinaweza kuhalalishwa vipi isipokuwa kwamba unakubaliana nao katika uadui na uhasama na dhidi ya taifa la Iran.

342/