Main Title

source : Parstoday
Jumanne

19 Desemba 2023

16:32:41
1421671

Afrika Kusini: Tutawavua uraia watakaokwenda kujiunga na safu za jeshi la utawala wa Kizayuni

Afrika Kusini imewaonya raia wake kwamba iwapo watakwenda kujiunga na safu za jeshi la Kizayuni vitani, watanyang'anywa uraia wao.

Tangu yalipoanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza mnamo tarehe 7 Oktoba, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na wananchi wa nchi hiyo wamekuwa wakionyesha mshikamano na wananchi wa Palestina.

Kwa mujibu wa Klabu ya Waandishi Habari Vijana , Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imesema imepata wasiwasi  mkubwa kutokana na  ripoti zinazoeleza kwamba baadhi ya raia wa nchi hiyo wanajiunga na jeshi la Kizayuni kwa ajili ya kwenda kupigana huko Gaza.

Wizara hiyo imesisitiza kuwa: hatua kama hizo zinaweza kuchangia ukiukaji wa sheria za kimataifa na kuunga mkono utendaji jinai za kimataifa.

Hapo awali Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imeeleza kwamba Idara ya Usalama wa Taifa inawafuatilia raia ambao wameajiriwa na Israel.

Mwezi uliopita, Afrika Kusini iliwasilisha ombi kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC la kuchunguzwa jinai za kivita za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Nchi hiyo pia iliwaita nyumbani wanadiplomasia wake kutoka Israel ili kutathmini uhusiano wake na utawala huo kwa kuzingatia idadi kubwa ya vifo vya raia huko Gaza.

342/