Main Title

source : Parstoday
Jumatano

29 Mei 2024

20:57:37
1462136

Donald Trump akiri juu ya udhaifu wa utawala wa Kizayuni

Donald Trump, Rais wa zamani wa Marekani amesema katika mkusanyiko wa Wayahudi wa Marekani kwamba utawala wa Israel umepoteza uwezo wake.

Gazeti la Washington Post limetoa ripoti kwamba Donald Trump, Rais wa zamani wa Marekani, amekiri kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ni dhaifu katika hafla ya kuchangisha fedha ya wafadhili wa Kiyahudi wa Marekani na kusema kuwa, anaunga mkono haki ya Israel ya kuendeleza mashambulizi huko ukanda wa Gaza.Katika miezi ya hivi karibuni wafadhili wa chama cha Republican wamemshinikiza Trump kuchukua msimamo mkali zaidi wa kuunga mkono utawala haramu wa Israel na Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.

Trump pia amejivunia sera zake kuhusu utawala haramu wa Israeli wakati alipokuwa Ikulu ya White House na kusema kuwa  utawala wa Israeli unahitaji msaada wake sasa kuliko wakati mwingine wowote.

Trump aliongeza kwa kusema kwamba, utawala huo wa Israel unapoteza nguvuu ake hata huko Washington na katika Kongresi.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umeshindwa kufikia malengo ya awali ya vita dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, na idadi ya wakosoaji wa sera na jinai za Netanyahu ndani na nje ya ardhi hiyo inayokaliwa kwa mabavu, inaongezeka kila siku.

Hadi sasa maafisa kadhaa wa ngazi za juu wa kijeshi na kijasusi wa utawala wa Kizayuni wamejiuzulu nyadhifa zao wakipinga siasa za Netanyahu. Taswira ya utawala huo bandia wa Kizayuni pia imezidi kuwa mbaya duniani kote hadi waitifaki na waungaji mkono wa muda mrefu wa utawala huo wamelazimika kubadili sera zao kuhusiana na utawala wa Israel 


342/