Main Title

source : Parstoday
Jumatano

17 Julai 2024

19:05:27
1472709

Bagheri Kani: Marekani ni kikwazo kikuu katika kuhitimisha mauaji ya kimbari ya Israel Ukanda wa Gaza

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameishutumu Marekani kwa vita vya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza. Ali Bagheri Kani amesisitiza umuhimu wa kushirikiana pande kadhaa ili kurejesha amani na utulivu duniani.

Ali Bagheri Kani ameeleza haya alipowasili New York huko Marekani kwa lengo la kushiriki katika mijadala miwili muhimu katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iliyoanza jana Jumanne na kuendelea leo Jumatano.  

Ajenda kuu za mkutano huo wa siku mbili wa Baraza la Usalama la UN ni kuhusu ushirikiano wa pande kadhaa na suala la Palestina.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa pande kadhaa duniani na kusema hatua na maamuzi ya upande mmoja ya Marekani si tu yameshindwa kudumisha amani, utulivu na usalama duniani bali matakwa ya kupinduka mipaka ya Marekani na sera yake ya mambo ya nje ya kutaka kutawala dunia vimesababisha mkwamo katika masuala muhimu ya kimataifa, mfano wa wazi ukiwa ni jinai zinazofanywa na Wazayuni huko Ukanda wa Gaza.

Bagheri Kani amesema ushirikiano wa nchi mbalimbali ndio njia mbadala na kusongeza kuwa: Iran ambayo ni nchi mwanachama wa kundi la BRCS na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) inaweza kuwa na nafasi na mchango athirifu na kwamba na itatumia uwezo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuangazia nafasi na umuhimu wa ushirikiano wa pande kadhaa ili kutatua masuala na matatizo mbalimbali ya kimataifa.

Amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatumia fursa hiyo kutetea haki za Wapalestina na kuweka wazi jinai za Israel. 

342/