Pezeshkian ameyasema hayo jana Jumatatu alipokutana na Katibu wa Baraza la Usalama la Russia Sergei Shoigu ambaye alikuwa mjini Tehran kwa ziara ya siku moja ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Iran. Amebainisha kuwa, Russia imekuwa mshirika thabiti katika nyakati za changamoto kwa Iran na kusisitiza ulazima wa kuharakisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya nchi hizo mbili. "Tunaamini kwamba enzi ya maamuzi ya upande mmoja yanayochukuliwa na madola fulani ikiwemo Marekani, imekwisha," amesema Rais Pezeshkian na kubainisha kuwa: "Mfungamano wa misimamo na ushirikiano kati ya Iran na Russia katika kujenga ulimwengu wa pande kadhaa bila shaka utaimarisha usalama na amani duniani."Ziara ya Shoigu hapa hapa nchini imefanyika huku kukiwa na mvutano mkubwa katika eneo hili la Asia Magharibi baada ya utawala wa kigaidi wa Israel kumuua Ismail Haniya, kiongozi wa kisiasa wa Hamas, mjini Tehran siku ya Jumatano iliyopita, na kulisukuma eneo kwenye ukingo wa vita.
342/