Abna - Sura Baqara, Aya 155:
«.وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنْفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ»
"Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri."
Mwenyezi Mungu huwajaribu wanadamu wote, lakini majaribio ya wanadamu hayafanani. Tunapaswa kujua kwamba mitihani ya Mungu ni kwa ajili ya kusitawisha vipaji na maendeleo ya mwanadamu. Zana za mtihani wa kimungu ni:
Matukio yote machungu na matamu, yakiwemo hofu na njaa, upotevu wa fedha na upotevu wa maisha na ukosefu wa bidhaa, hofu ya adui, mzingiro wa kiuchumi, vita na jihadi. Ili kushinda katika jaribu la hofu ya adui, tunahitaji kumtumaini na kumkumbuka Mungu, na ili kupigana na mapungufu, tunahitaji subira na ustahimilivu.
Sio lazima kwa watu wote kupimwa na masuala yote, lakini inawezekana kwa kila mtu kupimwa na kitu. Mtu anaweza kufaulu katika mtihani mmoja, lakini sio mwingine. Wakati mwingine mtihani wa mtu ni njia ya kuwajaribu wengine. Wakati mwingine kupunguzwa kwa mali na bidhaa au kuonekana kwa hofu na matatizo mengine ni kutokana na kupima kwa Mungu, lakini wakati mwingine, mambo haya ni matokeo ya matendo ya kibinadamu.
Wakati fulani wanadamu hufanya dhambi fulani ambazo Mungu huwapa shida fulani.
chanzo: alanwaralmunirah