Main Title

source : Abna
Jumatano

2 Oktoba 2024

13:15:33
1490874

Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati limedai na kuzitaka jumuiya za kimataifa kuchukua hatua ya kusitisha mashambulizi dhidi ya Lebanon.

Katika taarifa yake, Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati limelaani mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Lebanon na kupuuza Sheria za Kimataifa na Mikataba ya Geneva.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati limelaani vikali katika taarifa yake mashambulizi ya anga ya Utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Lebanon na kupuuza sheria za Kimataifa na Mikataba ya Geneva, na kutaka hatua za haraka zichukuliwe na jumuiya ya kimataifa ili kusitisha jinai hizo.

Baraza hilo liliongeza kuwa: Jeshi la Israel linaendesha mashambulizi ya anga katika maeneo ya Lebanon ambayo yanaelekea kuwa vituo vya Hezbollah, na mashambulizi haya yanaharibu vijiji vya Mashia na maeneo yenye Wakristo wengi.

Baraza la Makanisa limeashiria juu ya mazingira magumu ya kibinadamu na hali mbaya ya kibinadamu na kutangaza kuwa, maelfu ya watu wamekuwa wahanga na mamia ya maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao.

Baraza hili liliomba jumuiya ya kimataifa kutoa ulinzi wa kimataifa kwa raia na kutoa nyenzo na kinga muhimu kwa maisha ya binadamu.

Taarifa ya Baraza la Makanisa ilisema: "Hospitali kwa sasa ziko katika hali mbaya na haziwezi kutoa huduma kwa idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa, haswa wale waliojeruhiwa na milipuko."

Kwa mujibu wa Baraza la Makanisa la Mashariki ya Kati, wakati makanisa na shule vikiwa wazi kwa wakimbizi na misaada ya mtu mmoja mmoja kwa Wakristo na Waislamu ikiendelea kutolewa, hisia za kutoaminiana zipo miongoni mwa jamii tofauti na hii imeathiri juhudi za misaada.

Padri Rufael Zoghib, kasisi wa Kimaroni, alisema:

"Mashambulizi hayo yamepunguza hali ya kuaminiana na kuchochea mashaka".