Main Title

source :
Jumamosi

19 Machi 2011

20:30:00
293142

Makala ya Wiki

KUTEKWA KWA GILAD NI HATUA ZA MAFANIKIO KWA HAMAS

Gilad ni wajeshi wa Israel ambaye alitekwa na kupelekwa mafichoni na wanamgambo wa harakati za kutetea haki za nchi na wananchi wa madhulumu wa Parestina.

Tangu kutekwa kwake mapema Juni 25, 2006, Gilad Shalit aligeuka kuwa ndio turufu kubwa ya kundi la Hamas katika makabiliano yake na Israel. Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 alivushwa hadi Gaza baada ya shambulio la Hamas. Israel iliapa kumkomboa kwa nguvu zake zote na kuanzisha mashambulio ya kijeshi dhidi ya Gaza Palestina.Lakini pamoja na uwezo wa jeshi la Israel hawakufanikiwa kumkomboa. Hamas siku zote ilikuwa na sharti moja tu - kwamba wafungwa takriban 1500 wa Kipalestinina waachwe huru .Sharti hili liliwatia wasi wazazi wa Gilad ambapo mnamo mwaka 2007 baba yake Gilad Noam Shalit alikiri kwamba Sharti hilo ni vigumu kukubaliwa na Serikali ya ghasibu ya Israel.Yalifanyika maongezi ya pande mbili kwa muda ambapo Juhudi za upatanishi ziliongozwa na maafisa wa Ujerumani na Misri.walakini juhudi  zote ziligonga mwamba kutokana na kutokubaliwa shart la wanamgambo wa Hamasi.Wazazi ndugu na jamaa wa Gilad waliendeleza kampeni ya kushinikiza Gilad aachiliwe huru na kampeni hizi  zilizidi kupata msukumo na wito wa ajabu.Mapema mwaka 2009 Israeli ilianzisha mashambulio makubwa katika Gaza kwa lengo la kumkomboa Gilad Shalit lakini kutokana na msimamo wa wanamgambo wa Hamasi Jeshi la Israel halikufanikiwa. Na Badala yake walifikia makubaliano ya kuachiwa  kuachiliwa huru  wafungwa 20 wakike wa Kipalestina mukabala na video ya Gilad ambayo ilithibitisha kuwa bado yu hai.Gilad alionekana mdhoofu aliyekonda sana ingawa alikuwa na hali nzuri kiafya. Picha hizo zilisaidia kumfanya awe nembo kubwa zaidi  Israel ambayo siku zote imefanya juhudi kubwa za kuhakikisha kwamba inawarudisha wanajeshi wake waliotekwa, hata kama zitakuwa ni maiti.Lakini msemaji wa waziri mkuu mpya , Benjamin Netanyahu, bado alionekana  hataki kutekelezwa sharti la kundi la Hamas. Familia ya Gilad iliimarisha kampeni yake ya kufikiwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa wakiungwa mkono na vyombo vya habari vya Israeli na kuendeleza shinikizo kwa kuandamana kutoka nyumbani kwao hadi makao ya Bw: Netanyahu.Katika kipindi chote hicho Hamas haikuonyesha ishara yoyote ya kubadili msimamo wake.Hatimae Israel haikuwa na budi isipokuwa kukubaliana na sharti la kundi la Hamasi kwani maguvu hayakuwa na faida tena kwa Israel.Yafaa kuashiria kwamba waisrael walikubaliana na masharti hayo kwani waliona yalo watokea mwaka 2006 katika vita vya siku 33 kati ya Israel na Hizbolah ambapo Israel ilipata hasara kubwa kwani ilishambuliwa kwa makombora mengi ya Hizbollah na hatimaye kubadilishana mamia ya mateka wa Hizbollah mukabala na maiti za wanajeshi wa Israel, ambapo mpaka siku ya kubadilishana mateka Israel haikuwa na habari kwambawanajeshi wake walikuwa wamekufa tangu zamani.