Ayatollah Ramezani
-
Ayatullah Ramadhani: Bila ya Ghadir, Dini Ingepotoshwa Tangu Miaka ya Kwanza
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kwa kusisitiza nafasi ya kimkakati ya tukio la Ghadir katika kulinda asili na usafi wa dini, alisema: "Kama lisingekuwepo tukio la Ghadir, basi dini ingeweza kupotoshwa tangu miaka ya mwanzo."
-
Habari iliyoenea ya ufunguzi wa Ofisi ya ABNA nchini Ghana katika Vyombo vya Habari nchini Ghana
Sambamba na ufunguzi wa Ofisi ya kikanda ya Shirika la habari la ABNA nchini Ghana, vyombo vya habari vya nchi hiyo vilikaribisha uwepo wa chombo hiki cha habari cha kimataifa na kukitambulisha kama jukwaa la kusambaza simulizi za kitamaduni na kidini kutoka ulimwengu wa Kiislamu hadi Afrika Magharibi.
-
Ayatollah Ramezani: "Viongozi wa Dini wanapaswa kuwa waongozaji katika kufanikisha amani yenye haki"
Mkutano wa kihistoria wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ahlul Bayt (a.s) na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ivory Coast
Katika ziara ya Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ahlul Bayt (a.s) nchini Ivory Coast, alikutana kwa kifamilia na Kardinali Ignace Dogbo Assi, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini humo na mwakilishi wa Vatican. Katika mazungumzo hayo, pande zote mbili zilisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kidini, kuunga mkono heshima ya utu wa binadamu, na juhudi za kufanikisha amani ya kudumu duniani.
-
Ayatollah Ramezani: "Umoja wa Umma wa Kiislamu Ndiyo Njia ya Kukabiliana na Uonevu wa Kimataifa"
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Ahlulbayt (a.s) katika kongamano la "Wanafikra wa Dini; Kubadilishana Uzoefu na Teknolojia Mpya" alisisitiza umuhimu wa umoja wa Kiislamu, uenezi wa pamoja wa mafundisho ya Qur'an na Ahlulbayt (a.s), na utambuzi wa uwezo wa ndani.
-
Kauli ya Sheikh Omar Jane:
Kiongozi wa Jumuiya ya Maulamaa wa Senegal katika Kikao na Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (as):Iran Ipo Ndani ya Nafsi na Maumbile Yetu
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s), akiwa katika makao makuu ya Jumuiya ya Maulamaa wa Senegal, amesisitiza juu ya umuhimu wa umoja wa Kiislamu na kuimarisha uwezo wa kielimu na kidini katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema: “Umoja wa Kiislamu Ni Njia ya Kufikia Mamlaka ya Kiulimwengu”
-
Ayatollah Ramezani katika Sherehe (Hafla) ya Taklif ya Mabinti wa Senegal: Imani na Elimu ni Mabawa Mawili ya Kuruka (Kupaa) kwa Jamii ya Kiislamu
Kufanyika kwa Sherehe ya Kuvutia ya Taklif (Kufikia umri wa kutekeleza sheria za Kiislamu) kwa Mabinti wa Senegal Huko Dakar sambamba na uwepo wa Ayatollah Reza Ramezani
-
"Ayatollah Ramezani: Dini inapaswa kuwa na ufanisi katika nyanja mbalimbali za kitamaduni, kisiasa na kiuchumi"
"Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: Tunapaswa kuwa na mtazamo jumuishi kuhusu dini ili tuone athari kamili za dini; mtazamo jumuishi maana yake ni kwamba dini ina sura ya nje na ya ndani, ina wajibu wa mtu binafsi na pia wajibu wa kijamii. Haiwezekani dini iwe na hukumu nyingi za kijamii lakini isiwe na Serikali."
-
"Ayatollah Ramezani: Chuo cha Dini cha Qom kina uwezo wa kuunda ustaarabu wa Kiislamu / Mapinduzi ya Kiislamu yamebadilisha mlingano wa dunia."
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: Leo hii, fursa ya kipekee imepatikana kwa vyuo vya kidini, ambayo haijawahi kushuhudiwa katika vipindi vya nyuma. Tunapaswa kuweza kuitambulisha dini ya Uislamu kwa dunia kwa kutumia lugha na istilahi za kimataifa, na kwa hakika tutafaulu katika njia hii.