"Adui, kwa kushirikiana na Wamarekani, kila siku anaeneza mitego ya mauti kwa lengo la kuwaangamiza Wapalestina, na anaendelea kutekeleza uhalifu wa karne na fedheha ya enzi hii, kwa sababu amepewa uhakikisho kutoka kwa baadhi ya tawala za Kiarabu - bali anapewa motisha, msaada na uungwaji mkono nao."
Ayatollah Al-Udhma Abdullah Javadi Amoli alisisitiza umuhimu wa kuunganisha sanaa na ushairi na Tauhidi (umoja wa kumpwekesha Mwenyezi Mungu), akisema kuwa iwapo mafundisho ya tauhidi yatahuishwa kwa sura yake halisi, basi jamii ya Kiislamu haitapotea wala kukumbwa na vitisho kutoka kwa maadui.