-
Maelfu washiriki maandamano ya Arubaini ya Imam Hussein (as) katika Uwanja wa Imam Hussein mjini Tehran +Picha
Maandamano makubwa ya kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (as) yamefanyika katika Uwanja wa Imam Hussein (as) mjini Tehran, Iran, yakishirikisha maelfu ya waumini waliokusanyika kumuenzi mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) na kuhuisha ujumbe wa Karbala.
-
Maelfu Washiriki Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein (as) katika Jimbo la Kano, Nigeria +Picha
Maelfu ya Waislamu na wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) wameendelea kushiriki matembezi ya Arubaini katika Jimbo la Kano nchini Nigeria, wakihuisha ujumbe wa A'shura na kuwakumbuka Mashahidi wa Karbala pamoja na waathiriwa wa shambulio la mwaka 2014.
-
Maelfu ya wanafunzi washiriki maombolezo ya Arubaini karibu na eneo la kuuawa kwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei +Picha
Maelfu ya wanafunzi kutoka jumuiya mbalimbali za vyuo nchini Iran wamekusanyika kuadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (as), ambapo walisoma Ziyarat al-Arbaeen na kumuenzi Ayatullah Sayyid Ali Hosseini Khamenei katika eneo lililotajwa kuwa mahali alipouawa.
-
Wanafunzi wa Afrika Wanaosoma Nchini Iraq Wakutana na Ayatollah Ramezani Kujadili Uenezi wa Mafundisho ya Uislamu Barani Afrika +Picha
Wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za Afrika wanaosoma nchini Iraq wamekutana na Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), Ayatollah Reza Ramezani, ambapo walijadili njia za kuimarisha shughuli za tablighi na kueneza mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) katika Bara la Afrika.
-
Mapokezi na Mazishi ya Mwili wa Shahidi Brigedia Jenerali wa Pili Rubani Majid Kazemi mjini Shiraz +Picha
Mwili wa Brigedia Jenerali wa Pili Rubani Shahidi Majid Kazemi, mmoja wa marubani mashujaa wanne wa ndege za kivita za Sukhoi Su-24 wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ulipokelewa kwa heshima katika Kituo cha Anga cha Shahid Doran mjini Shiraz. Shahidi Kazemi alifariki shahidi akiwa njiani kurejea Iran baada ya kushiriki katika operesheni ya kijeshi dhidi ya Kambi ya Al Udeid nchini Qatar, ambayo kwa mujibu wa taarifa iliharibu miundombinu na vifaa vya kijeshi vya Jeshi la Marekani.
-
Hawzah ya Hazrat Zainab (s.a) Yaandaa Darasa la Tafsiri ya Qur’an na Maombolezo ya Imam Hussein(a.s) Kuhusu Changamoto za Vita vya Kisaikolojia +Picha
Shule ya Wasichana Hazrat Zainab (s.a.) iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam, imeandaa darasa la Tafsiri ya Qur’ani Tukufu pamoja na maombolezo ya Imam Hussein (a.s.), ambapo washiriki walijadili athari za vita vya kisaikolojia katika kudhoofisha fikra, imani na maadili ya vijana.
-
Wanafunzi Hawza ya Hazrat Zainab (sa) Washiriki Katika Maombolezo ya Imam Hussein (a.s) na Mashahidi wa Karbala +Picha
Wanafunzi Mabinti 144 wa Hawzah ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo chini ya Jamiat Al-Mustafa - Tanzania, pamoja na wasimamizi wao, wamehuisha Majlisi ya kuomboleza Shahadat ya Imam Hussein (a.s) na Mashahidi wa Karbala, ikiwa ni siku ya 30 ya maombolezo yanayo endelea katika Hawzah ya Mabanati ya Hazrat Zainab (sa).
-
Vipande 62 vya Mabaki ya Miili ya Wanafunzi Waliodhulumiwa wa Minab vimepatikana na kufanyiwa vipimo vya DNA
Vipande 62 vya mabaki ya miili ya wanafunzi wa Minab vimefanyiwa vipimo vya DNA na kubainika kuwa ni vya watu 32.
-
Chuo cha Kimataifa cha Al-Mustafa (s) Dar es Salaam Chaendelea Kuimarisha Elimu ya Qur'an Tukufu +Picha
Darasa la mafunzo ya Qur'an Tukufu limeendelea katika Chuo cha Kimataifa cha Al-Mustafa (s) Jijini Dar es Salaam, Tanzania likiongozwa na Al-Haj Sheikh Muhammad Ja'far huku usomaji wa Qur'an ukifanywa na Sheikh Khamis Mpili.
-
Iraq yatangaza vituo vya mipakani kwa raia wa kigeni na wahamiaji watakaoshiriki Arubaini ya Imam Husayn (as)
Serikali ya Iraq imetangaza taratibu za kuingia na kutoka nchini kupitia vituo maalumu vya mipakani kwa raia wa kigeni na wahamiaji wanaokusudia kushiriki ibada ya Arubaini ya Imam Husayn (as) katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.
-
Waumini Nakuru, Kenya Waadhimisha Kumbukumbu ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran kwa Dua na Maombolezo +Picha
Waumini mjini Nakuru nchini Kenya wamekusanyika katika hafla ya maombolezo na dua kwa ajili ya kumkumbuka kiongozi wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakieleza mshikamano wao na kutoa heshima kwa mchango wake katika kutetea waliodhulumiwa na kusimamia misingi ya Uislamu na haki.
-
Marasimu ya Maombolezo na Kumbukumbu ya Imam Shahidi Yaandaliwa katika Haram ya Bibi Fatima Ma'suma (s.a) Qom +Picha
Sherehe ya kuenzi kumbukumbu ya Imam Shahidi, Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu ainue daraja lake), imefanyika katika Haram Tukufu ya Bibi Fatima Masuma (a.s.) mjini Qom, kwa mwaliko wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Shule ya Wasichana Yaadhimisha Shahada ya Imam Sajjad (a.s.) kwa Majlisi ya Maombolezo +Picha
Majlisi ya maombolezo ya kumbukumbu ya shahada ya Imam Ali ibn al-Husayn As-Sajjad (a.s.) imefanyika katika Shule ya Wasichana, ambapo washiriki 144 walihudhuria na kupata mawaidha kuhusu maisha, subira na urithi wa Imam wa Nne wa Ahlul-Bayt (a.s.).
-
Tazama Waombolezaji Walivyodhihirisha Mapenzi ya Dhati kwa Shahidi Sayyid Ali Hussein Khamenei (ra) Wakisubiri Kuwasili kwa Mwili Wake +Picha
Waombolezaji walikesha katika maeneo ya mazishi wakiwa wamelala huku wakikumbatia picha za Shahidi Sayyid Ali Hussein Khamenei (ra), wakionyesha upendo wao wa dhati na uaminifu kwa kiongozi wao walipokuwa wakisubiri kuwasili kwa mwili wake ili watoe heshima za mwisho.
-
Mwili wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Mashahidi wa Familia Yake Wawasili Mashhad Ukisindikizwa na Ndege za Kivita +Video
Ndege za kivita za Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimesindikiza ndege iliyobeba mwili wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi pamoja na mashahidi wa familia yake, kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Shahid Hashemi Nejad mjini Mashhad, huku maandalizi ya mazishi yakiendelea.
-
Kisa cha Kihistoria:Jinsi na Kwa Nini Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad Aliuawa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq /MEK
Kwa mujibu wa simulizi za kihistoria, kuuawa kwa Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad mnamo mwaka 1981 kulikuwa sehemu ya mfululizo wa mauaji yaliyotekelezwa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq (MEK), likiwa na lengo la kuwaondoa viongozi waliokuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
-
Hali na Matukio mbalimbali ya Karbala Jinsi Yalivyokuwa Wakati wa Kumpokea Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei (ra) +Picha
Mji Mukufu wa Karbala jana ulitawaliwa na huzuni kubwa na hali ya maombolezo pindi Waumini walipokuwa wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Ayatollah Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei (ra) kwa ajili ya shughuli za kutoa heshima zao za mwisho.
-
Wanafunzi wa Jamiat AlMustafa(s)Tanzania Washiriki Mazishi ya Ayatollah Imam Sayyid Ali Khamenei(ra) Wakifuatilia Moja kwa Moja Kupitia Mtandao+Picha
Wanafunzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Al-Mustafa nchini Tanzania walifuatilia kwa njia ya matangazo ya moja kwa moja (live) kupitia mtandao ibada ya mazishi na maziko ya Ayatullah Imam Sayyid Ali Khamenei mjini Mashhad, wakionesha mshikamano na kuwapa pole wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Swala ya Maiti Yasalishwa kwa Mwili wa Ayatollah Sayyid Ali Husseini Khamenei katika Haram ya Amirul Muuminiin (a.s.) mjini Najaf + (Video 7 +Picha 4)
Swala ya maiti ya Ayatollah Sayyid Ali Husseini Khamenei imesaliwa katika Haram Tukufu ya Amirul Muuminiin Imam Ali (a.s.) mjini Najaf, chini ya uongozi wa Ayatollah Sayyid Muhammad Taqi Al-Hakim, huku waumini na wanazuoni wengi wakihudhuria kumuombea rehema na kutoa heshima zao za mwisho.
-
Mwili wa Kiongozi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei Wafikishwa katika Haram ya Imam Hussein (a.s.) Karbala +Picha
Mwili mtukufu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei, pamoja na miili ya mashahidi wa familia yake, umefikishwa katika Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) mjini Karbala, ambako maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo.
-
Malawi: Waumini Wakamilisha (Kisomo) Khatmu ya Qur'an Tukufu kwa Ajili ya Roho na Nafsi ya Shahidi Sayyid Ali Khamenei +Picha
Waumini nchini Malawi wamekusanyika katika Shule ya Al-Hadi chini ya uwakilishi wa Al-Mustafa kufanya Khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kumuombea Shahidi Sayyid Ali Khamenei.
-
Viongozi wa Dini na Serikali Waungana na Mamilioni ya Wananchi Katika Mji wa Qom kushiriki Mazishi ya Shahidi Sayyid Ali Khamenei +Picha
Maulamaa, wanazuoni, viongozi wa kidini na serikali pamoja na mamilioni ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Iran wamekusanyika katika mji wa Qom kushiriki marasimu ya mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Taifa, Shahidi Sayyid Ali Khamenei.
-
Mamilioni Wafurika Qom Kumuaga na Kumuenzi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei +Picha
Mamilioni ya waombolezaji walikusanyika katika Msikiti wa Jamkaran mjini Qom kushiriki katika marasimu ya kumuaga na kumuenzi Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, huku Sala ya Maiti ikiongozwa na Ayatollah Javadi Amoli.
-
Maelfu na Mamilioni ya Waombolezaji Washiriki Katika Mazishi ya Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei nchini Iran+Picha
Mamilioni ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya Iran na baadhi ya nchi nyingine walijitokeza kushiriki katika mazishi ya Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, wakionesha heshima, mapenzi na mshikamano wao kwa Kiongozi huyo.
-
Dunia Yashuhudia Mamilioni ya Waombolezaji Wakimzika Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei +Picha
Mamilioni ya watu walifurika katika mitaa ya mji mkuu wa Tehran kushiriki mazishi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, pamoja na baadhi ya wanafamilia wake waliouawa na kufikia daraja ya shahada.
-
Upendo wa Kitaifa na Kimataifa | Maelfu Waendelea Kumiminika Jijini Tehran - Iran Kumuenzi Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei +Picha
Maelfu ya waombolezaji kutoka Iran na mataifa mbalimbali duniani wameendelea kufika kuanzia jana (Jumamosi) alfajiri hadi usiku ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei, wakimkumbuka kwa unyenyekevu wake na msimamo wake wa kutetea wanyonge, hususan wananchi wa Palestina.
-
Waombolezaji waaga Mwili Mtukufu wa Kiongozi Shahidi katika Msala wa Imam Khomeini Jijini Tehran +Picha
Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza katika Msala wa Imam Khomeini (Quds Sirruh) mjini Tehran kutoa heshima zao za mwisho na kuuaga mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei (Qudsallahu Nafsahu Az-Zakiyyah), katika mazingira ya huzuni na majonzi makubwa.
-
Hali ya Majonzi Yatanda Tehran sambamba na kuanza kwa Shughuli za Kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Hali ya majonzi na huzuni kubwa imeendelea kutawala katika mji wa Tehran kuelekea shughuli za mwisho za kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei(Ra), huku umma wa Kiislamu ukiendelea kutoa heshima zake kwa Kiongozi huyu Mwema na mtetezi wa Haki za Wapalestina na Haki za wanyonge popote walipo Ulimwenguni.
-
Rais wa Iran Akutana na Ujumbe wa Nje Uliohudhuria Shughuli za Maombolezo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu +Picha
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na ujumbe mbalimbali wa nchi za nje uliohudhuria shughuli za maombolezo ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ambapo walisisitiza mshikamano na nafasi yake katika Umma wa Kiislamu.
-
Kibaha - Pwani | Waumini wa Shia Kibaha Wafanya Matembezi ya Amani ya A'shura, Wasisitiza Ujumbe wa Haki na Kupinga Dhulma+Picha
Mamia ya Waumini wa Madhehebu la Shia Ithna Ashari katika Mji wa Kibaha, Mkoani Pwani, wamefanya Matembezi ya Amani ya A'shura kwa Mwaka wa 1448 H - 2026 kwa lengo la kuhuisha kumbukumbu ya Shahada ya Imam Hussein (AS) na kuendeleza mafunzo ya haki, uadilifu na kupinga dhulma.