24 Januari 2020 - 07:36
Brian Hook amchimba mkwara Esmail Ghaani

Mwakilishi na mwanasheria mkubwa wa Marekani kunako masuala ya Iran Bw Brian Hook, katika kinachoelezwa kuwa ni ishara ya kujifaharisha na vitendo vya kigaidi ameibuka na kutishia maisha ya kiongozi wa sasa wa Jeshi la Quds la Iran Esmail Ghaani ambaye amechukua nafasi ya Qasem Suleimani.

Shirika la habari la Ahalu Bayt (as):

Mwakilishi na mwanasheria mkubwa wa Marekani kunako masuala ya Iran Bw Brian Hook, katika kinachoelezwa kuwa ni ishara ya kujifaharisha na vitendo vya kigaidi ameibuka na kutishia maisha ya kiongozi wa sasa wa Jeshi la Quds la Iran Esmail Ghaani ambaye amechukua nafasi ya Qasem Suleimani.

Katika mazungumzo yake Bw Hook amenukuliwa akisema kuwa Esmail Ghaani kama ataamua kufuata na kupita njia alizokuwa akipita Qasem Suleimani basi na yeye yatamkuta yaliyomkuta Qasem Suleimani.

Kauli ya Hook imeonekana kuwa ni kama kutetea kila ambacho Marekani iliyafanya dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa Jeshi la Quds Shahidi Qasem Suleimani.

Vitisho hivi vinakuja baada ya Esmail Ghaani kunukuliwa akielezea tukio la kuuwawa kwa Qasem Suleimani na usema kuwa ni kitendo ambacho ni kinyume na sheria na wala si cha watu mashujaa.

“...Waliomuua Qasema Suleimani hawakuwa watu wa mapambano katu, na kama wangekuwa ivyo basi wangalimfuata katika uwanja wa vita. Lakini katika hali ya kinyume na maadili kabisa wakaamua kumfanyia ugaidi, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na nguvu za walipiza kisasi kote ulimwenguni, tutahakikisha pia maadui hawa wanapigwa...” aliweka wazi Esmail Ghaani.