(ABNA24.com) Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Nchi Kavu cha IRGC alisema hayo jana Jumanne na kuongeza kuwa, wanachama wa genge hilo la kigaidi wanaoendesha harakati zao katika maeneo ya mipaka ya kaskazini magharibi, magharibi na kusini mashariki mwa Pakistan wamepokea mashehena ya silaha kutoka Riyadh.
Amesema kundi hilo la kigaidi limepokea kwa uchache ndege tatu zilizosheheni silaha, jambo ambalo linadhihirisha bayana kuwa, magenge ya kigaidi Asia Magharibi yanaungwa mkono kikamilifu na Marekani, Saudia na vibaraka wao katika eneo.
Brigedia Jenerali Mohammad Pakpour ameeleza bayana kuwa, licha ya kupata uungaji mkono wa hali na mali, lakini vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimeendelea kutoa vipigo kwa magenge hayo ya kigaidi.
Kundi la kigaidi la Jaishul Adl la Pakistan limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mabomu na utekaji nyara ndani ya Pakistan na kusini mashariki mwa Iran, katika mpaka wa nchi mbili hizi za Kiislamu.
.............
340