29 Machi 2020 - 07:22
Rais Hassan Rouhani asisitiza kutekelezwa kikamilifu mipango yote ya kukabiliana na Corona

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ili kukabiliana na virusi vya Corona, ni lazima kutekelezwa kikamilifu na kwa uangalifu mpango wa mtengano wa kijamii nchini Iran.

(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo Jumamosi katika kikao cha kamati ya kitaifa ya kusimamia na kukabiliana na virusi vya Corona mjini Tehran na kuongeza kuwa, kupitishwa mpango huo wa utengano wa kijamii utaendelea hadi tarehe 20 Farvardin inayosadifiana na tarehe 8 Aprili.

Amefafanua kuwa watu wote na vyombo vya utekelezaji nchini Iran ni lazima viwe na ushirikiano katika kukabiliana na Corona. Aidha kwa mara nyingine Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, wananchi wa Iran wako katika mazingira magumu ya vikwazo na dunia inaendelea kushangazwa ni namna gani nchi ambayo iko chini ya vikwazo imeweza kusimama imara katika kukabiliana na virusi angamizi vya Corona.

Tangu mwanzo kuliporipotiwa virusi vya Corona nchini Iran, kulianza kutekelezwa hatua za kuzuia na za matibabu kwa msaada wa jeshi na vyombo vyote husika na hadi sasa hatua za kuwatenga wagonjwa (kuwaweka karantini) na kuwatibu waathirika wa Corona zingali zinaendelea kutekelezwa kwa haraka kupitia ushirikiano wa watu wote.

Mpango wa kuweka utengano wa kijamii ambao pia una lengo la kukata msururu wa kusambaa maradhi hayo, kupitia kuzuia mikusanyiko na kufuta safari zote zisizo za dharura nchini, ulianza kutekelezwa Ijumaa asubuhi.

...........
340