7 Mei 2020 - 10:55
Polisi ya Rwanda yawakamata watu 1,400 jijini Kigali kwa kukiuka 'kafyu ya corona'

Watu 1,400 wametiwa nguvuni na polisi katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali kwa kukiuka agizo la kutotoka nje usiku, kama moja ya hatua ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hayo yalisemwa jana Jumatano na John Bosco Kabera, msemaji wa Jeshi la Polisi la Rwanda ambaye ametoa onyo kali kwa wale watakaopuuza maagizo yaliyotolewa na serikali kwa ajili ya kuzuia kuenea ugonjwa wa Covid-19.

Amesema miongoni mwa waliokamatwa kwa kupatikana wakiwa nje katika muda wa kafyu kuanzia saa mbili usiku hadi kumi na moja alfajiri, iliyotangazwa Jumatatu iliyopita ni waendeshaji magari na wenye kutembea kwa miguu.

Msemaji wa Polisi ya Rwanda amesema watakaobainika kuwa walikiuka agizo hilo la kut

Kabla ya hapo serikali ya Rwanda iliweka sheria ya kutotoka nje kote nchini humo ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona, lakini baadhi ya wakazi wamekuwa wakilalamika juu ya ukatili wanaofanyiwa na maafisa wa usalama wanaosimamia utekelezwaji wa sheria hiyo.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Rwanda, watu 268 walikuwa wameambukizwa virusi vya corona nchini Rwanda kufikia jana Jumatano, na hakuna aliyepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo nchini humo. Aidha idadi ya wagonjwa wa corona waliopata afueni nchini humo imeongezeka na kufikia watu 130.

otoka nje usiku bila sababu za msingi watatozwa faini au watazuiliwa kwa siku kadhaa.

342/