Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Rais Rouhani ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa miradi kadhaa ya nishati kwa njia ya video. Amesema kuwa, uzinduzi wa miradi hiyo ni jibu madhubuti kwa uadui wa Marekani na Israel watenda jinai.
Amesema maandamano ya sasa ya Wamarekani dhidi ya ubaguzi wa rangi ni kielelezo kwamba, Marekani imo katika kipindi kibaya zaidi cha historia yake na kuongeza kuwa, raia weusi wanasumbuliwa na dhulma kubwa nchini humo.
Ameashiria mauaji yaliyofanywa na polisi wa Marekani dhidi ya raia mwenye asili ya Afrika, George Floyd, na kusema kuwa hii ni kadhia ya kimataifa inayoonesha mshikamano baina ya wanadamu. Amesema tukio hilo linaonesha kwamba, dunia bado ina njia ndefu hadi kufikia kwenye ustaarabu uliosisitizwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ametangaza mshikamano wake na raia wa Marekani na kusema: Mienendo ya serikali ya Marekani na ikulu ya rais wa nchi hiyo, White House ambayo ndiyo iliyotoa amri ya kufanyika jinai hizi, inapaswa kulaani.
Vilevile amekosoa hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kutumia kitabu cha Biblia kwa ajili ya kuhalalisha jinai na ukatili wa serikali yake na kuwahadaa Wamarekani na akasema: Biblia haiamuru kufanya mauaji ya watu wasio na hatia na ni aibu kuona rais anayekandamiza raia wake wa Marekani akishika mkononi kitabu cha Injili. Rais Rouhani aesisitiza kuwa Waislamu wanaiheshimu Injili na Nabii Issa Masiih (as).
342/